Thursday 8 August 2013

SYRIA NA MACHAFUKO YAKE


Syria yakana msafara wa Asaad umeshambuliwa



 

 Syria imekanusha ripoti za mashambulio dhidi ya msafara wa rais Bashar al-Assad alipokuwa akielekea msikitini Kaskazini Magharibi mwa mji mkuu Damascus kuhudhuria ibada ya sherehe za Idd Il Fitr zinazokamilisha mwezi mtukufu wa Ramadhani .

Wanaharakati na wakaazi wa eneo hilo walisema kuwa mabomu kadhaa yalianguka katika eneo hilo , na taarifa kutoka upande wa waasi wa Free Syrian Army zinasema kuwa msafara wake ulishambuliwa.

Televisheni ya taifa nchini Syria ilionyesha picha za video za rais Assad akitabasamu , huku akisalimiana na maafisa alipowasili katika msikiti kwa ajili ya kushiriki sala ya Idd .

Huku baadhi ya watu waliotoa maoni yao kwenye mtandao wa Tweeter wakishuku kuwa picha hizo zilirekodiwa kabla , ni dhahiri hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa bwana Assad alipata madhara yoyote.
Waziri wake wa mawasiliano , amekanusha vikali taarifa za shambulio dhidi ya msafara wa rais akitaja shutuma hizo kama ''ndoto'' .

Amesema kuwa Bwana Assad aliendesha gari lake mwenyewe kuelekea kwenye msikiti na kila kitu kilikuwa katika hali ya kawaida.

Lakini baadhi ya wanajeshi katika jeshi la Syria walisema kuwa makombora yalirushwa katika eneo alikokuwa wakati huo yakilenga msafara wake .

Wakazi wa eneo hilo pia waliunga mkono madai hayo wakisema walisikia milio ya milipuko mapema asubuhi.

Kwa vyovyote vile yaelekea bwana Assad amenusurika .

Hii ni mara ya tatu kwa bwana Assad kuonekana hadharani katika kipindi cha wiki moja, jambo ambalo lisingeweza kufanyika miezi kadhaa iliyopita wakati mji mkuu Damascus ulipokuwa ukishambuliwa mara kwa mara

TINDIKALI ZANZIBAR



Waingereza washambuliwa Zanzibar


Ni mara ya kwanza kwa shambulizi kama hili kutokea Zanzibar

Polisi katika kisiwa cha Zanzibar wamesema wanawake wawili wa Uingereza wamerushiwa maji ya Acid katika nyuso zao baada ya kuvamiwa mwendo wa usiku.

Naibu kamishna wa polisi amesema kuwa wanaume wawili waliwatendea wanawake hao Katie Gee na Kirstie Trup, wote wenye umri wa miaka 18 kutoka London,kitendo hicho walipokuwa wakitembea katika barabara za mji wa kihistoria wa zanzibar.

Wanawake hao ni walimu wa kujitolea wakifanya kazi kisiwani humo

Amesema kuwa polisi tayari wameanzisha msako dhidi ya wanaume hao. 

Katika taarifa yake shirika la usafiri la i-to-i nchini Uingereza lilisema kuwa wanawake hao wameondoka hospitalini.

Kwa upande wake wizara ya mambo ya ndani Uingereza ililezea wasiwasi kuhusu mashambulizi dhidi ya raia wake na kuwa tayari imetoa msaada kwao kupitia kwa ubalozi wake.

Wanawake hao, wanasemekana kufanyia kazi shirika moja la kujitolea na nia ya shambulizi hilo haijulikani.
Polisi wanasema kuwa wanawake hao wenye umri wa miaka 18 walikuwa wakitembea katika mji wa Mawe kisiwani Zanzibar ambao ni kivutio kikuu cha utalii kisiwani humo, wakati wanaume wawili waliokuwa wamepanda piki piki walipowamwagia Acid kwenye mikono , vifua na nyuso zao.

Wanawake hao walipelekwa kwa ndege hadi Dar es Salaam ambako walipokea matibabu . Afisa wa wizara ya afya amesema kuwa majeraha yao si ya kutishia maisha .

Polisi wa Zanzibar wamesema ni mara ya kwanza kwa raia wa kigeni kushambuliwa kwa namna hiyo na kwamba wanawasaka wahusika.

Zanzibar ni kisiwa kinachokaliwa na idadi kubwa ya waislam na shambulio hilo linakuja katika kipindi cha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan , wakati watu wakisherehekea sherehe za Eid

BAADA YA KULIPUKA KWA MOTO KWENYE UWANJA NDEGE HUKO KENYA



Shughuli katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata zarejea katika hali yake ya kawaida.


Habari hizi na mashirika ya habari

Shughuli katika uwanja wa kimataifa wa ndege JKIA nchini Kenya, zinatarajiwa kurejea katika hali ya kawaida kuanzia usiku wa manane.

Waziri wa usafiri, Michael Kamau, amesema kuwa sehemu iliyotengewa marasia kuingilia na kutoka kwenye uwanja hyuio itatumiwa na wageni kutoka nchi za kigeni watakaowasili katika uwanja huo.

Safari kadhaa za ndege za kimataifa zilirejea leo huku ndege za shirika la ndege la Kenya zikitua na kuruka katika hali inayoweza kusemekana kuwa ya kawaida.

Ndege za kimataifa zimeanza kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa jijini Nairobi JKIA, siku moja tu baada ya kitengo cha kuwasili wageni kuchomwa na moto mkubwa na kulazisha uwanja huo kufungwa kwa masaa kadhaa.

Ndege ya kwanza ya kimataifa kuwasili katika uwanja huo ni ile iliotoka Uingereza na baadaye nyengine kutoka Tanzania na Bangkok zikawasili.

Wachunguzi hata hivyo wanatathmini chanzo chake.

Wakati huo huo Rais wa Marekani, Barack Obama amesema ataisaidia serikali ya Kenya katika kukarabati uwanja huo wa ndege baada ya moto mkubwa kuuteketeza hapo jana.

Katika ujumbe wake wa simu, Obama alisisitiza kuwa Marekani iko tayari kuisadia Kenya katika hali ile yoyote kutokana na ushikiano wake na Kenya.

Obama pia aliwapa pole familia zilizowapoteza wapendwa wao katika mashambulizi ya bomu ya Agosti 1998 mjini Nairobi.

Manmo Jumatano, moto mkubwa uliotokea majira ya asubuhi, uliharibu kitengo cha kuwasilia wageni wa kimataifa.

Vikundi vya wachunguzi viliwasili katika uwanja huo kufanya uchunguzi wao kubaini kilichosababisha moto huo.

Abiria walikwama kutokana na mkasa huo ingawa waliweza kuondolewa nje ya uwanja kwa ajili ya usalama wao huku baadhi wakiangalia mizigo yao ikiteketea wasijue la kufanya. .

Rais Uhuru Kenyatta aliwasili katika uwanja huo na kujionea uharibifu uliotokea na kiisha kutoa taarifa yake kupitia kwa msemaji wake Esipisu aliyesema kuwa chanzo cha moto huo kinachunguzwa.

Wapelelezi wanaendelea na uchunguzi kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata mjini Nairobi, kufuatia moto mkubwa uloanza Jumatano alfajiri na kuteketeza jengo la mapokezi ya abiria wa kimataifa.


KUELEKEA KINDUMBWENDUMBWE CHA LIGI KUU YA SOKA YA ENGLAND.


 “Wayne Rooney hayuko kifedha zaidi” Owen.



 

           Na. deo kaji makomba

Maamuzi ya mhambuliaji wa timu ya soka ya Manchester United, Wayne Rooney ya eidha  kubaki katika klabu hiyo yenye masikani yake Old Traford hayatachochewa na fedha, hiyo ni kwa mujibu wa mchezaji mwenzake wa zamani Michael Owen.

Rooney tayari amehusishwa mchakato wa kutaka kuondoka ndani ya klabu hiyo ya mashetani wekundu,licha ya klabu hiyo iliyo chini ya kocha mpya hivi sasa David moyes, ikisisitiza kuwa Roney hauzwi.
Owen aliiambia BBC Sport, “Wayne Rooney hayuko kwa ajili ya kutaka kulipwa malipo makubwa. Yuko kwa minajili ya kucheza soka.

“Anapenda sana mpira, na si fedha. Anataka kuwa akicheza soka muda wote katika mashindano makubwa.”

Owen mwenye umri wa miaka 33, alicheza na Rooney katika timu ya taifa ya England pamoja na klabu ya Manchester united kabla ya kutundika daruga kuachana na soka mwishoni mwa msimu uliopita.

Anaamini kuwa Roney mwenye umri wa miaka 27, anapenda kubaki Old Trafford lakini anahofia hana muda mrefu kubakia katika chaguo la kikosi cha kwanza ndani ya Manchester United.

Rooney hakuhusishwa ndani ya kikosi katika ligi ya mabingwa kilichofungwa na Real Madrid hapo mwezi machi na meneja mpya wa Manchester United, David Moyes, akieleza kuwa Rooney hatokuwa katika chaguo lake katika kikosi cha kwanza, mapema katika wakati huu wa kiangazi huku Robin Van Persie akionekana ni mshambuliaji namba moja katika kikosi cha kwanza cha mashetani hao wekundu.

United wamekwishakataa ofa mbili kutoka Chelsea ikiwemo ile yenye thamani ya pauni milioni 25 na nyongeza nyingine

Owen amesema: “Kiuhakika Wayne atapenda kubaki Machester United, akicheza kila mchezo. Swali kubwa hapa Manchester United itampa uhakika wa kuwemo katika kikosi cha kwanza?

“Nashindwa kuelewa kwanini watu wanazungumza  pesa wakati wote. Wayne Rooney yuko sawa katika suala la pesa na hakuna mtu anayetakiwa kuwa na wasiwasi kuhusiana na kipato kuongezeka.
“Baada ya kumjua kwa muda mrefu Rooney  na naweza kukuhakikishia hayuko kifedha

KUELEKEA KINDUMBWENDUMBWE CHA LIGI KUU YA SOKA YA ENGLAND.



Sakata la Luis Suarez kutaka kuikacha Liverpool kuelekea Asernal;

·     Bosi wa Liverpool Brendan Rodgers, amtaka Suarez kujikosoa



·     Asema Suarez ameonesha dharau kubwa licha ya kupewa kila kitu na klabu hiyo.

        Na. deo kaji makomba.

Mshambuliaji wa timu ya soka ya Liverpool, Luis Suarez, ametakiwa na bosi wa klabu hiyo, Brendan Rodgers kujikosoa na kujifunza yeye mwenyewe, na kuongeza kuwa Suarez ameonesha dharau kubwa kwa majogoo hao wa Anfeld.

Rodgers pia amepinga madai ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay  ya kwamba aliahidiwa ataondoka ndani ya klabu hiyo katika msimu huu wa kiangazi endapo kama Liverpool haitashinda katika ligi ya mabingwa barani ulaya.

Suarez mwenye umri wa miaka 26, yuko katika mpango wa kuwasilisha maombi yake ya uhamisho wiki hii kama mchakato wake wa kuelekea kwa washika bunduki wa London, Asernal the Gunners, utazuiliwa na uongozi wa Liverpool.

“Hakukuwa na ahadi yoyote iliyotolewa na hakuna ahadi iliyovunjwa.” Alisisitiza Rodgers.
“Klabu na mwakilishi wa mchezaji huyo, wamekuwa na mazungumzo na alijua sahihi wapi alikuwa.
“Amekuwa dharau ya hali ya juu kwa klabu, klabu ambayo ilimpatia mchezaji huyo kila kitu.” Alisema bosi huyo wa Liverpool.