Thursday 8 August 2013

SAKATA LA MKASA WA MOTO ULIOTOKEA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA JOMO KENYATA MJINI NAIROBI



Wapelelezi waendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha mkasa wa moto huo.

Na. deo kaji makomba na mashirika ya habari

Wapelelezi wanaendelea na uchunguzi kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata mjini Nairobi, kufuatia moto mkubwa uloanza Jumatano alfajiri na kuteketeza jengo la kuwasilia abiria wa kimataifa.

Wakati huo huo safari za ndege za ndani ya nchi zilianza jioni ya Jumatano kufuatana na katibu wa mawasiliano Ezekiel Mutua alipozungumza na Sauti ya Amerika. Anasema wanatarajia safari za Kimataifa kuanza alhamisi asubuhi lakini taarifa rasmi itatolewa na maafisa wa serikali karibuni.

Bw. Mutua anasema hadi jumata no jioni wapelelezi hawakujua kilichosababisha moto huo na kueleza kwamba maafisa wa usalama na kikosi cha kupambana na ugaidi wamekuwa wakikutana siku nzima na kufanya uchunguzi wao kutokana na tetesi kwamba kulikuwepo na malalamiko kadhaa kwenye uwanja huo wa kimataifa.

Maafisa wanasema mashahidi 120 kutoka idara ya usafiri wa anga ya kenya na uhamiaji wamehojiwa. Abiria elfu 16 wameathiriwa na ajali hiyo iliyosababisha hasara ya mamilioni ya shilingi.



No comments:

Post a Comment