Tuesday 27 August 2013

MAONESHO YA NANE YA BIASHARA YA KIMATAIFA

Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara mkoa wa Mwanza, TCCIA, Bw. Elibariki Mmari, akizungumzia mandalizi kuelekea maonesho ya Nane ya biashara kwa nchi za ukanda wa Afrika mashariki, mbele ya wandishi wa habari katika ukumbi wa kipepeo uliopo kwenye hotel ya new Mwanza, juamanne hii



Maonesho ya biashara kwa nchi za Afrika mashariki kufanyika jijini Mwanza.

·        Ni kuanzia Agost 30 mwaka huu.


·        Bidhaa za makampuni mbalimbali kutoka nchi za Afrika mashariki kuwa kivutio katika maonesho hayo.


·        Zaidi ya makampuni 350 kushiriki maonesho hayo.



                         

                                              Na. deo kaji makomba.


Zaidi ya makampuni ya biashara 350 yanatarajia kushiriki katika maonesho ya biashara ya afrika mashariki  yanayotarajia kuanza agost 30 mwaka huu kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana jijini Mwanza.

Makampuni kutoka nchi za ukanda wa afrika mashariki, ikiwemo Kenya, Uganda na mwenyeji Tanzania yatashiriki katika maonesho hayo yaliyofikia mwaka wa nane tangu kuanza kwake, yakiandaliwa  na chama cha wafanyabiashara nchini Tanzania, mkoa wa Mwanza, TCCIA.

Akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa kipepeo uliopo kwenye hotel ya New Mwanza, mwenyekiti  wa TCCIA mkoani Mwanza, Bw. Eribaliki Mmari, amesema kuwa licha ya makampuni kutoka ukanda wan chi za afrika mashariki pia makampuni kutoka nchi za China, Misri pamoja na Singapore yatashiriki katika maonesho hayo makubwa.

Kulingana na Bw. Mmari, bidhaa zitakioneshwa  katika maonesho hayo ni bidhaa zitokanazo na kilimo, chakula na vinywaji, viwanda vya nguo, bidhaa zitokanazo na ushonaji pamoja na ufumaji.
 Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mwanza, Bw. Mmari, akiwiwa na viongozi wenzake wakati wa mkutano na wandishi wa habari.

Bidhaa zingine zitakazooneshwa katika maonesho hayo ni bidhaa kutoka viwandani pamoja na huduma zitolewazo na makampuni mbalimbali ya mawasiliano na teknolojia nchini Tanzania.

Akizungumzia mafanikio tangu kuanzaishwa kwa maonesho hayo mnamo mwaka 2005, mwenyekiti huyo wa TCCIA mkoani Mwanza, amesema kuwa kumekuwepo na mafanikio makubwa  yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwake ikiwemo mafanikio binasfi ya makampuni mbalimbali ambayo yamekuwa yakishiriki katika maonesho hayo, pamoja na serikali kupitia taasisi zake.

Akitolea mfano Bw. Mmari, amesema kuwa maonesho hayo yametoa fursa kwa wawekezaji mbalimbali nchini Tanzania, kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo mahotel.
 Picha ikionesha moja ya hotel yenye hadhi ya nyota tano iliyoko katikati ya jiji la Mwanza katika makutano ya barabara za Kenyata na Posta.(Picha zote na deo kaji makomba)

Bw. Mmari ameongeza kusema kuwa maonesho hayo ya biashara kwa nchi za ukanda wa Afrika mashariki yanatoa fursa kwa makampuni yaliyoko nchini Tanzania na jumuiya ya afrika mashariki kuweza kutangaza bidhaa zao.

Maonesho hayo pia yanatarajia kutoa fursa kwa makampuni mbalimbali ya biashara nchini Tanzania kuweza kujifunza na kuongeza uuzaji nje bidhaa kwa ajili ya kuwa tayari kupata faida katika masoko ya kidunia yaliyoandaliwa ikwemo AGOA, EPA, pamoja EBA.