Wednesday 9 September 2015

WATUKUTU WA STAND CHAMA LA WANA WAULA


Description: Description: cid:image001.jpg@01D0E7B4.C93E0980

Mwenyekiti wa stand united Amani Vicent (kushoto) akibadilishana mkataba wa udhamini wa timu hiyo na Makamu wa rais wa ACACIA anaeshugulikia masuala ya Kampuni, Deo Mwanyika mara baada ya kutiliana saini mkataba wa miaka miwili na kampuni hiyo.
 

ACACIA YAIDHAMINI TIMU YA STEND UNITED KWA BILIONI MOJA

·        Ni udhamini mnono wa miaka miwili.
·        Udhamini huo umelenga kukuza soka kwa vijana.

Ijumaa, Septemba, 4th 2015: Kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Acacia iliingia mkataba wa miaka miwili na timu ya Stend United ya Mkoani Shinyanga kwa ajili ya kushiriki ligi kuu ya Vodacom ambayo inategemewa kuanza tutimua vumbi katikati ya mwezi huu. Stand United ni moja kati ya timu bora kabisa katika kanda ya ziwa ambayo imeshiriki katika ligi kuu msimu uliopita 2014/2015 na kumaliza ikiwa nafasi ya tisa.

Udhamini wa ACACIA katika misimu hii miwili ya ligi kuu itasaidia katika kuifanya timu ya Stand United iweze kufanya vizuri katika michezo yake, pamoja na kusaidia katika kuboresha programu mbalimbali za timu na kuendeleza vipaji pamoja na masuala ya Utawala.
 Description: Description: cid:image002.jpg@01D0E7B4.C93E0980
Aman Vincet, mwenyekiti wa timu ya Stand United kushoto na Deo Mwanyika kulia ambaye ni makamo wa rais wa uendeshaji wa shughuli wa kampuni ya Acacia, wakionesha mkataba mbele ya wageni waalikwa katika hafla fupi ya kutiliana saini kuidhamini timu yake katika hotel ya Vigmark mjini shinyanga.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Makamu wa rais wa Acacia aneshughulikia masuala ya kampuni, Deo Mwanyika, amesema  “Kwa takriban mwaka mmoja, tumekua tukifanya kazi pamoja na Stand United. Kwa muda huo tulianzisha mchakato wa kutambua namna nzuri ya kuboresha ushirikiano wetu ili kunufaisha watu wa Shinyanga na Kanda ya Ziwa kwa ujumla.

Bwana Deo amesema Msimu uliopita uliwapatia fursa nzuri ya kushuhudia uwezo wa timu hiyo hasa ukizingatia ilikua mara yao ya kwanza kushiriki ligi kuu, “Baada ya tathmini ya kina, tunadhani huu ni muda muafaka wa sisi kusaini makubaliano au mkataba wa kuidhamini na kufanya kazi pamoja ya kuikuza timu hii ya nyumbani maarufu kama “Chama la wana”.
 Description: Description: cid:image003.jpg@01D0E7B4.C93E0980
 Baadhi ya wachezaji wa Stend United wakionyesha jezi watakazotumia msimu huu wa ligi kuu ya Vodacom mara baada ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali na wadhamini wao kampuni ya ACACIA. Kutoka kushoto ni Seleman Mrisho, Frank Hamis,Shabani Dunia, Geremia Enos, Jonh Mwenda na Kheri Khalfan

Hivyo, Leo, Acacia tunasaini mkataba na timu ya Stand United kwa udhamini wa misimu miwili ya ligi kuu, wenye thamani ya Shilingi bilioni moja. Udhamini huu unajuamuisha shughuli za uendeshaji wa timu, kuboresha uongozi na kukuza vipaji.
 Description: cid:image037.jpg@01D0E7DF.5D38C830
 Wachezaji wa Stend United wakionyesha jezi yao itakayokuwa ikitumika kwa michezo ya uwanja wa nyumbani na ile ya ugenini wakati wa msimu wa ligi kuu ya Vodacom.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Stand United Amani Vincent, amesema udhamini huo wa miaka miwili utakuwa chachu kwa timu yake kufanya vizuri katika ligi kuu, “Msimu uliopita tulimaliza tukiwa nafasi ya nane na kipindi hicho hatukuwa na fedha ya kutosha kuendesha timu, lakini kwa udhamini tulioupata kutoka kwa ndugu zetu wa Acacia vijana wetu safari hii watafanya vizuri zaidi.
 Description: cid:image039.jpg@01D0E7DF.5D38C830

 Description: cid:image041.jpg@01D0E7DF.5D38C830
 Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Ali Nassoro Lufunga akikabidhiwa jezi na makamo wa rais wa Acacia Deo Mwanyika, kabla ya kuanza kwa mechi kati ya Stand United na Olympic Stars ya Burundi kwenye uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Description: cid:image042.jpg@01D0E7DF.5D38C830
 Kikosi cha Acacia Stand United, kikipasha moto misuli kabla ya mechi dhidi ya Olympic Stars, ambapo Acacia Stand United chama la wana waliibuka washindi kwa bao 1-0
 Description: cid:image032.jpg@01D0E7DF.5D38C830
 Baadhi ya washabiki wa Stend United waliohudhuria wakati wa uzinduzi wa jezi mpya za timu hiyo ikiwa pia ni sehemu ya kusherekea udhamini wao na kampuni ya Uchimbaji wa madini ya ACACIA.

Kampuni ya Acacia ni kampuni inayoongoza kwa shughuli za uchimbaji wa madini hapa Tanzania huku ikiwa na Migodi mitatu katika kanda ya ziwa, kupitia mradi wa “Acacia Maendeleo Fund” ambao ndio pia umetoa udhamini wa timu ya Stend umekuwa pia ukitekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa Jamii hapa nchi huku kampuni hiyo ikieleza kuwa dhamira yake ni kuendelea kufanya kazi na Jamii zinazowazunguka katika kuwaletea Maendeleo wenyeji.