Sunday 23 June 2013

CONFEDARATION CUP


BRAZIL YAIFYATUA ITALIA, MEXCO YAIPIGA JAPANI.

LEO USIKU NI NIGERIA NA UISPANIA, URUGUAY NA TAHIT MECHI ZA KUNDI B


Na. Deo Kaji Makomba

Hekaheka za kuwania kombe la mabara inazidi kuhika kasi huko nchini Brazil, huku timu za mataifa manane zikiendelea kuchuana katika ile hatua ya makundi.

Jumamosi kulishuhudiwa mechi mbili za kundi A zikipigwa huku zikizihusisha timu nne zilizoko katika kundi hilo Brazil, Italia, Mexco na japani.

Matokeo katika kundi hilo hao jana, Brazil iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Italia wakati Mexco iliishinda Japani 2-1.

Msimamo katika kundi A, mara baada ya mechi mbili za jana jumamosi usiku
                                          

Confederations Cup Group A


P
W
D
L
Pts
GD







Brazil 3 3 0 0 9 +7
Italy 3 2 0 1 6 +0
Mexico 3 1 0 2 3 -2
Japan 3 0 0 3 0 -5


Hekaheka hizo za kuwania kombe la mabara zinaendelea tena usiku wa leo huko nchini Brazil, huku kukishuhudiwa mechi mbili za kundi B zikichezwa.

Wawakilishi wa bara la Afrika, timu ya taifa ya Nigeria inashuka dimbani kupambana usokwauso na timu ya taifa Uispania, wakati Uruguay na Tahit nazo zitakuwa zikioneshana kazi..
 Kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Nigeria, kinachoshiriki mashindano ya mabara huko Brazil


Nigeria inaingia uwanjani hii leo kama nyati aliyejeruhiwa, baada ya kukubali kipigo cha mabao2-1 katika mchezo wake uliopita dhidi ya Uruguay, lakini itakuwa ikipambana na miongoni mwa kigogo cha soka duniani, timu ya taifa ya Uispania ambayo inaingia uwanjani huku ikiwa inatakata na ushindi  wa mabao 10-0 dhidi ya timu ya taifa ya Tahit




KATIKA SOKA ‘HUKO MAJUU’


TOTTENHAM YAWEKA DAU MEZANI KUMSAJILI KIUNGO WA KIMATAFA WA BRAZIL.


·        Ni Paulinho, anayekipigia Corinthians

·        Aweka hadhari kuwepo na mpango huo wa Tottenham, lakini asema...

  

 Na. Deo Kaji Makomba.


Kiungo wa kimataifa wa Brazil Paulinho, ameweka hadaharani kuwa, klabu cha kandanda cha Tottenham Hopas cha England,  kimefanya taratibu kisheria kuhusu kumpatia ofa ya kuichezea klabu hiyo, lakini ataamua majaliwa yake mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Confederation Cup.

Mchezaji huyo wa Corinthian mwenye umri wa miaka 24, ameiambia BBC Sport ya kwamba anakubaliana na ofa hiyo lakini hakuna kilicho na hakika.

Akizungumza mara baada ya ushindi iliyoupata Brazil wa mabao 4-2 dhidi ya Italy, alisema; “Kuna ofa kiofisi kutoka Tottenham kwenda Corinthians.

“Lakini kama nilivyofanya wakati ule katika ofa ya Inter Milan, nitaketi na kuamua pamoja na familia yangu kabla sijafanya maamuzi yoyote.”

Paulinho, hakucheza mechi ya jumamosi iliyopita kutokana na kuwa na jeraha katika kifundo cha mguu, wakati timu yake ikiitandika mabao 4-2 uitalino.

Kiasi cha dau anachotarajiwa kupewa kiungo huyo, chaelezwa kuwa ni pauni milioni 17.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil amekwishakuichezea timu yake ya taifa mechi 15, na huku akiifungia timu yake ya taifa magoli manne, ukiunganisha na goli moja alilofunga katika ushindi wa 3-0 katika michuano ya Confedaration Cup dhidi ya Japan wiki iliyopita.