Tuesday 23 July 2013

STARS NDANI YA MWANZA


HARAKATI ZA KUWANIA TIKETI YA KWENDA AFRIKA KUSINI HAPO MWAKANI KATIKA FAINALI ZA CHAN.

·        Stars yaendelea kujifua Mwanza

·        Kuondoka jumatano hii kwenda kupambana na shughuli pevu ya waganda.

                           Na. Deo Kaji Makomba.

Kikiosi cha timu ya soka ya  taifa ya Tanzania, Taifa tars, kinazidi kujifua vilivyo, kikiwa katika kambi yake jijini Mwanza, ikiwa ni mandalizi ya mchezo wake wa marudiano dhidi ya timu ya taifa ya Uganda The Cranes, utakaopigwa siku chache zijazo huko mjini kampala nchini Uganda.

Mchezo huo ni wa marudiano wa kuwania tiketi ya kucheza michuano ya kombe la CHAN, inayoshirikisha wachezaji wa soka wanaocheza ligi za ndani barani Afrika, ambapo fainali zake msimu huu zikitarajia kufanyika huko nchini Afrika ya kusini.

Takribani siku tatu hivi kikosi hicho cha stars, kiko Jijini Mwanza kikijaribu kujiweka sawa kiufundi  chini ya kocha wake mkuu Kim Poursen , ikiwa ni pamoja na kuzoea hali ya hewa ya Mwanza ambayo inaendana na hali ya hewa ya mjini Kampala, huko Uganda.



Makipa wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, taifa stars, wakiongozwa na Juma    Kaseja aliyeko katikati wakipiga jalambe uwanja wa CCM Kirummba, kujiandaa na mechi dhidi ya Stars huko kampala.

Stars hiyo inayoshiriki michuano ya CHAN, inajiandaa kwenda kupambana na The Cranes ya Uganda, huku ikiwa na kumbukumbu ya kichapo cha bao 1 -0 kutoka kwa timu hiyo, katika harakati za mwanzo tu kuwania tiketi ya kuelekea nchini Afrika ya Kusini hapo mwakani, kwenye mchezo uliopigwa wikiendi iliyopita jijini Dare es salaam.

Mchezo huo wa marudiano utakaofanyika  wikiendi hii huko mjini Kampala, Uganda,  untarajiwa kuwa wa vutanikuvute kutokana na timu zote kutaka ushindi ili kuweza kusonga mbele.

Kwa msingi huo stars yapaswa kuuchukulia mchezo huo kwa umakini zaidi, ikiwemo kurekebisha makosa yaliyojitokeza kiufundi katika mchezo wa awali, ili iweze kuwakomalia Waganda na pengine kuwafunga mabao2 -0 ili kuweza kuwa na matumaini ya kusonga mbele katika harakati hizo za kuwania kucheza fainali za CHAN hapo mwakani huko nchini Afrika ya kusini.

Kikosi hicho cha stars kimepiga kambi katika hotel ya Lakailo Jijini Mwanza.
Kikosi hicho cha Tanzania (Taifa Stars)  kinaondoka Mwanza jumatano hii (Julai 24 mwaka huu) kwenda Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la CHAN itakayochezwa Jumamosi (Julai 27 mwaka huu) Uwanja wa Mandela kuanzia saa 10 kamili jioni.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Mwanza chini ya Kocha Kim Poulsen tangu Julai 14 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza Fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
                           
                          "wacha nami niuze sura kwa mzungu"....Tegete
Meneja wa uwanja wa CCM Kirumba, John Tegete, akiteta jambo na                    kocha mkuu wa Stars Kim Poulsen, wakati Stars ilipokuwa mazoezi jumatatu hii kwenye uwanja wa CCM Kirumba. (Picha zote na Deo Kaji Makomba)

Timu hiyo itaondoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza saa 7.25 mchana kwa ndege ya PrecisionAir, na inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe.

HARAKATI ZA KUWANIA UBINGWA LIGI KUU YA SOKA YA VODACOM TANZANIA BARA.



·        TFF yatoa ratiba, kivumbi kuanza kutimka agost 24
·        Timu zote 14 kufungua pazia la michuano hiyo. 

                  Na.  Deo Kaji Makomba.

 Hekaheka za kuwania ubingwa wa ligi kuu yasoka ya Vodacom Tanzania bara, zinatarajia kuanza hapo mwezi agost 24 mwaka huu, huku kukishuhudiwa jumla ya timu 14 zinazoshiriki ligi hiyo zikiingia katika viwanja tofauti kukata utepe katika ligi kuu hiyo ya msimu huu.

Lakini kabla ya kuanza kwa kindumbwendumbwe hicho cha ligi kuu ya soka Tanzania bara, kutakuwa na mechi ya kufungua msimu (Ngao ya Jamii- Community Shield) kati ya bingwa mtetezi Yanga na Makamu bingwa Azam itakayochezwa Agosti 17 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi za Agosti 14 mwaka huu zitakuwa kati ya Yanga na Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Mtibwa Sugar na Azam (Uwanja wa Manungu, Morogoro), na JKT Oljoro na Coastal Union (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).

Nyingine ni Mgambo Shooting na JKT Ruvu (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers na Simba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Kagera Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Ruvu Shooting na Tanzania Prisons (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani).