Wednesday 14 August 2013

BADO NI HATARI HUKO NCHINI MISRI

Afisa wa usalama wa Misri anazungumza na mwanamke anaeshikilia mti katika kambi iliyoshmabuliwa na vikosi vya usalama. karibu na chuo kikuu cha Cairo huko Giza, Cairo, Misri, Jumatano
Afisa wa usalama wa Misri anazungumza na mwanamke anaeshikilia mti katika kambi iliyoshmabuliwa na vikosi vya usalama. karibu na chuo kikuu cha Cairo huko Giza, Cairo, Misri, Jumatano


Misri yatangaza amri ya dharura

  •  Yaelezwa watu 2,200 wameuwawa
  •  Jeshi laamrishwa kusaidia kutanzua mzozo
 

                    Na. deo kaji makomba,
                         na mashirika ya habari


Serikali ya Misri imetangaza amri ya dharura nchini kote kuanzia hii leo jumatano, kwa muda wa mwezi moja kufuatana na taarifa ya rais iliyotangaza na televisheni ya taifa.

Taarifa hiyo ina liamrisha pia jeshi kukisaidia kikosi cha polisi ili kuweza kutanzua mzozo huo unaotapakaa kote Misri.

Taarifa hiyo imetolewa wakati vikosi vya usalama vilikuwa vinashambulia makambi mawili kuwaondowa wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani bwana Mohamed Morsi katikati ya mji mkuu wa Cairo.

Wakati huo huo kumekuwepo na ripoti zinazotofautiana hii leo juu ya idadi ya watu walouliwa na walojeruhiwa katika ghasia zinazotokea kote nchini.

 Wizara ya afya inaeleza watu 95 wameuliwa na wengine 974 kujeruhiwa kote nchini.

hata hivyo baadhi ya wanachama wa chama cha Muslim Brotherhood cha Bw Morsi wanasema idadi ya walofariki imefikia hadi 2,200 na wengine elfu 10 kujeruhiwa.

MAAFA YATOKEA INDIA


Picha ikionesha Nyambizi ya India ikiwa imezama na waokozi wakionekana kuendelea na shughuli ya uokozi, picha kwa hisani ya Reuters

Maafa yatokea India.     

  • Ni baada ya Nyambizi kuzama
  • Ni ile iliyofanyiwa marekebisho miezi mitatu iliyopita na kugharimu dola milioni 8



                 Na. deo kaji makomba,
                           na mashirika ya habari


Habari kutoka Mumbai, India, zinasema kuwa waokoaji waliopiga mbizi kuwatafuta manusura hawajapata chochote.

 Mkuu wa jeshi la wanamaji nchini India D. K Joshi amesema kuwa watu 18 walikuwa kwenye nyambizi iliyozama baada ya kukumbwa na milipuko miwili mikubwa.

Waziri wa Ulinzi wa India A. K . Anthony ametaja tukio hilo kama baya zaidi kuwahi kutokea kwa wanamaji wa nchi hiyo. Iliwachukua wazima moto masaa kadhaa kuzima moto ambao ulionekana katika nyambizi.

Ripoti kutoka eneo la tukio hilo zinasema kuwa wanamaji kadhaa waliruka kutoka kwenye nyambizi kuokoa maisha yao baada ya mlipuko.

 Waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali maalumu ya wanamaji. 
Maafisa wakuu wa idara ya wanamaji wamesema kuwa sehemu moja 
ya nyambizi hiyo ilikuwa imezama majini na eneo lingine kuchomeaka kabisa.

Nyambizi hiyo iliyotengenezewa Urusi ilifanyiwa marekebisho miezi mitatu iliyopita kwa gharama ya Dola Miloni 8.