Picha ikionesha Nyambizi ya India ikiwa imezama na waokozi wakionekana kuendelea na shughuli ya uokozi, picha kwa hisani ya Reuters
Maafa yatokea India.
- Ni baada ya Nyambizi kuzama
- Ni ile iliyofanyiwa marekebisho miezi mitatu iliyopita na kugharimu dola milioni 8
Na. deo kaji makomba,
na mashirika ya habari
Habari kutoka Mumbai, India, zinasema kuwa waokoaji waliopiga mbizi kuwatafuta manusura hawajapata chochote.
Mkuu wa jeshi la wanamaji nchini India D. K Joshi amesema
kuwa watu 18 walikuwa kwenye nyambizi iliyozama baada ya kukumbwa na milipuko
miwili mikubwa.
Waziri wa
Ulinzi wa India A. K . Anthony ametaja tukio hilo kama baya zaidi kuwahi
kutokea kwa wanamaji wa nchi hiyo. Iliwachukua wazima moto masaa kadhaa kuzima
moto ambao ulionekana katika nyambizi.
Ripoti kutoka
eneo la tukio hilo zinasema kuwa wanamaji kadhaa waliruka kutoka kwenye
nyambizi kuokoa maisha yao baada ya mlipuko.
Waliojeruhiwa wamepelekwa katika
hospitali maalumu ya wanamaji.
Maafisa wakuu wa idara ya wanamaji wamesema kuwa
sehemu moja
ya nyambizi hiyo ilikuwa imezama majini na eneo lingine kuchomeaka
kabisa.
Nyambizi hiyo iliyotengenezewa Urusi
ilifanyiwa marekebisho miezi mitatu iliyopita kwa gharama ya Dola Miloni 8.
No comments:
Post a Comment