Friday 14 June 2013

HABARI MAHSUSI




Ajali ya Tren na bus yatokea Shinyanga muda mfupi uliopita
 


Habari zilizotufikia hivi punde hapa katika chumba chetu cha habari cha mtandao huu kutoka mjini Shinyanga magharibi mwa Tanzania, zinaarifu ya kuwa kuna ajali mbaya imetokea ikilihusisha basi la abiria Sai Baba lililokuwa likitokea Jijini Dare es salaam kuelekea Jijini Mwanza kugongana na gari moshi la abiria lililokuwa likitokea Jijini Mwanza kuelekea Dare es salaam.
Kulingana na vyanzo vya habari kutoka katika eneo la tukio, vinaeleza ya kuwa ni ajali mbaya imetokea huku majeruhi wakiokolewa na hakuna taarifa yoyote endapo kama kuna watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo
Tunafanya juhudi za kumtafuta kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga Bwana Mangala Evarist ili kupata undani wa taarifa hii. Endelea kufuatila mtandao huu.

TASINIA YA MUZIKI WAKIZAZI KIPYA YAPATA PIGO TENA.


·     Baada ya kufariki Mangwea, Langa naye “achomoka.”
Na. Deo Kaji Makomba.

Tasinia ya muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, imepatwa pigo jingine baada ya kuondokewa na mwanamuziki  mwingine ikiwa ni siku chache tu baada ya kuzikwa kwa mwanamuziki Albert Mangwea, aliyefariki dunia huko nchini Afrika ya kusini na kuzikwa mkoani Morogoro.

Mwanamuziki aliyefariki dunia wakati huu  ni Langa Kileo, almaarufu Langa, mzee wa matawi ya juu.

Taarifa zilizopatika hapo jana majira ya jioni kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii, na kukifikia chumba chetu cha habari cha mtandao huu ,zimeeleza kufariki dunia kwa mwanamuziki huyo ambaye pia aliwahi kufanya vyema katika tasinia ya muziki wa kizazi kipya wakati ule akichomoka akiwa na kundi zima la wakilisha.

Langa akiwa na kundi hilo aliweza kutikisa na wimbo wao wa Kiswangilishi, huku akiendelea kutamba na rekodi nyingine ikiwemo ile iliyojulikana kwa jina la matawi ya juu.
Kabla ya kifo cha mwanamuziki huyo kutokea, alikuwa akitamba na rekodi mpya aliyoitoa takribani wiki mbili zilizopita, rekodi iliyojulikana kwa jina la rafiki wa kweli.
Kifo cha Langa, kimetokea katika hospital ya rufaa ya Muhimbili, ambapo mwili wa marehemu, umehifadhiwa huko na taratibu za mazishi zikiendelea kufanyika.