Wednesday 10 July 2013

MICHUANO YA SOKA YA WACHEZAJI WANAOCHEZA LIGI ZA NDANI BARANI AFRIKA, (CHAN)

UGANDA THE CRANES KUTUA KESHO (ALHAMIS) KUPAMBANA USOKWAUSO NA STARS, UWANJA WA TAIFA.


Na. Deo Kaji makomba.



 Timu ya soka ya Taifa ya Uganda (The Cranes) inatarajiwa kuwasili nchini kesho alhamis(Julai 11 mwaka huu) tayari kwa mechi ya kwanza ya mchujo kusaka tiketi ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ilioyotolewa na shirikiho la soka nchini Tanzania, TFF,na kisima cha habari kupata nakala yake,The Cranes inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 5.30 asubuhi kwa ndege ya Air Uganda ambapo itafikia hoteli ya Sapphire iliyoko maeneo ya Kariakoo, jijini Dare es salaam.

Wakati huohuo,Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limefanya mabadiliko ya mwamuzi wa mechi ya mchujo kusaka tiketi ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The Cranes) itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwamuzi aliyeondolewa kutokana na sababu za kiufundi ni Jean Claude Birumushahu aliyekuwa mwamuzi msaidizi namba moja, huku nafasi yake sasa inachukuliwa na Herve Kakunze pia kutoka Burundi.

CAF imemuondoa mwamuzi huyo baada ya kufeli katika mtihani wa waamuzi (Cooper Test) kwa waamuzi wa Burundi wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) uliofanyika nchini humo siku tatu zilizopita.

Wakati huo huo, makocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen na wa Uganda, Milutin Micho pamoja na manahodha wao watakuwa na mkutano na Waandishi wa Habari utakaofanyika keshokutwa (Julai 12 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF kuzungumzia mechi ya Jumamosi.