Tuesday 5 November 2013

TIDDO MGENI RASMI TUZO YA MWANGOSI

Marehemu Daudi Mwangosi.

   Muungano wa klabu za wandishi wa habari Tanzania, UTPC kutoa tuzo ya Mwangosi kila mwaka.

  • Ni ya uandishi wa habari za kishujaa na utumishi uliotukuka.

  • Tiddo Muhando kuwa mgeni rasmi .

  • Mshindi katika tuzo hiyo kujinyakulia shilingi milioni 10 .        


                                     Na. Mashaka Baltazar. 



MKURUGENZI wa Kampuni ya Mwananchi Comunication Ltd, Danstun Tiddo Mhando atakuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo ya Mwangosi ya Uandishi wa Habari za Kishujaa na Utumishi uliotukuka.

Tuzo hiyo imeanzishwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na itaolewa Novemba  mwaka huu, ambapo mshindi atazawadiwa shilingi 10 milioni na cheti na itatolewa, Septemba 2 ya kila mwaka.

Marehemu Mwangosi aliuawa na polisi kwa kupigwa bomu tumboni,Septemba 2, 2012 katika kijiji cha Nyololo, Mkoani Iringa wakati akitekeleza majukumu yake ya uandishi wa habari .

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza jana , Rais wa  UTPC,Kenneth Simbaya, alisema tuzo hiyo ya kishujaa itakuwa ya kumuenzi marehemu Mwangosi  na waandishi wengine waliojitoa kulitumikia taifa lao kwa maslahi ya jamii.

“Tuzo hii imepewa jina la Daud Mwangosi,inatolewa kwa mara ya kwanza hapa nchini  katika historia ya tasnia ya habari, ili kuwaenzi na kuwatambua waandishi wa habari ambao wanateswa,wanadhaliliswa, kupigwa na hata kuuawa kwa ajili ya kutekeleza kazi zao za kitaaluma,” alisema Simbaya.

Alisema marehemu Mwangosi ni mwandishi wa kwanza wa habari kuuawa hapa nchini wakati akifanya kazi yake,hivyo ni wajibu wa wana habari wote Tanzania kuwaongoza wapenda amani kumuenzi na kummbuka dama .

Pia alieleza kuwa ni wajibu wa wana habari kwa umoja wetu, kupaza sauti kulaani kwa nguvu zetu zote, unyama aliofanyiwa marehemu Mwangosi na ni matarajio kuwa wote wataungana na UTPC kuhakikisha mkondo wa sheria unachukua nafasi yake, ili haki yake ipatikane.

“waandishi wa habarri wanafanya kazi ya kuihabarisha jamii na wanawajibka kwayo.Wanapata mateso kwa jamii hiyo,hivyo tumeona tutoe tuzo hiyo Novemba 7 mwaka huu, hafla ambayo itafanyika JB Belmonte hoteli mbele ya umma wa Watanzania,”alisema Simbaya

Alisema wageni 120 kutoka ndani na nje ya Tanzania akiwemo mke wa marehemu Mwangosi watahudhuria hafla ya utoaji wa tuzo hiyo, ambapo mgeni rasmi atakuwa Mkurugenzi wa Mwananchi Communication Ltd Danstun Tiddo Mhando.

Aidha Rais huyo wa UTPC kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi na Viongozi wa klabu za waandishi wa habari nchini ,aliwashukuru Majaji kwa kazi nzuri ya kumchagua mshndi wa tuzo hiyo na kuwataja kuwa ni Mwenyekiti Nkwabi Mwanakilala na wajumbe,Leila Sheikh,Hamza Kassongo na Dkt Ayoub Ryoba.

Wakati huohuo Mkurugenzi wa UTPC Abubakar Karsan,amesema kuwa umeanzishwa mfuko wa Media Support Development Fund,utakaosaidia Waandishi wa habari watakaopata madhara wakitekeleza majukumu yao ya kitaaluma.

Alisema mafuko huo utatoa msaada wa kisheria kwa wanahabari watakaofikishwa mahakamani wakitekeleza majukumu yao,tiba kwa watakaojeruhiwa kazini na kuwasaidia uhamisho kutoka maeneo wanakofanyia kazi baada ya kupata matatizo.

Kuhusu msaada kwa familia ya marehemu Mwangosi, Karsan alisema kamwe UPTC haiwezi kujisifu kwa unyama uliofanywa ubaradhuri mmoja kwa kutoa roho ya Mwangosi, na kwa muktadha huo, ndiyo sababu ya umeanzishwa mfuko wa kuwasaidia waandishi wa habari watakapopatwa na matatizo wakiwa kazini.