Thursday 13 June 2013

MTANZANIA ANAYEFANYA MUZIKI WA HIP HOP NCHINI MAREKANI,AACHILIA HEWANI MWANAHIP HOP WA KWELI.

                                                   
·      Ni Ardo King Simple,atikisa Chicago katika katika show.
·      Mwana Hip Hop wa kweli aitoa kama zawadi kwa watanzania na Afrika Mashariki.
         
Na. Deo Kaji Makomba

Mtanzania anayeishi na kufanya shughuli zake nchini Marekani,Eliatosha Adonia, almaarufu,  Ardoking Simple, ameachilia hewani kibao chake kipya alichokirekodi katika mahadhi ya Hip Hop huko nchini Marekani.

Kibao hicho kijulikanacho kwa jina la Mwana Hip Hop wa kweli, kutoka chini ya lebo ya Legendary Music Inc(Chicago-U.S.A and Japan), kimeruhusiwa kuruka hewani na management nzima ya Legendary Music Inc, inayosimamia na kuratibu  kazi za mwanamuziki huyo, mwenye asili ya Jiji la Miamba na Sangara,(The rocky city) Mwanza Tanzania.
Tayari kibao hicho kimeanza kusikika hewani tangu tarehe 11 mwezi huu wa sita mwaka huu katika vituo mbalimbali vya radio nchini Tanzania.

Akizungumza katika wavuti yake kabla ya rekodi hiyo haijaruka hewani kama utambuliho wa kazi zake ambazo hivi sasa ameamua kuzifanyia nchini Marekani akishirikiana na wanamuziki mbalimbali nchini humo, licha ya kuwa amefanya baadhi ya rekodi nyingine kwa lugha ya kimombo, Ardo king amesema kuwa Single ya Mwana Hip Hop, ameirekodi kwa lugha ya kiwahili ikiwa na malengo ya kuwapa kitu kitu roho inapenda watu wa nyumbani Tanzania, lakini pia kuitangaza lugha nadhimu ya Kiswahili kimataifa zaidi.

Kama ilivyo kwa wanamuziki wengine, ana matumaini na ana matarajio makubwa kwa Single yake ya Mwana Hip Hop itatikisa na kufanya vyema katika vituo mbalimbali vya radio pamoja na mitaa mbalimbali hapa nyumbani Tanzania, na Afrika Mashariki.

Ardo King Simple, ameongeza kusema kuwa ana matarajio na anaamini katika uwezo wake wa ubunifu wa mashairi yake akitaka kuwahika mahabiki wa Hip Hop.
Kabla ya mwanamuziki huyo kutoa hewani rekodi hiyo mpya na kuiachilia katika vituo mbalimbali vya radio nchini Tanzania siku tatu zilizopita, amesema maendeleo yake kimuziki kiukweli anamshukuru mungu kuona yanakwenda vizuri, baada kuwepo nchini Marekani kwa takribani miaka mitano iliyopita, na kuona ndoto zake zinaendelea vyema.
Akizungumza katika mahojiano maalum na safu yetu ya burudani katika mtandao huu, Ardoking Simple, amesema kuwa miezi takribani mine iliyopita alifanya show ya muziki mjini Chikago nchini Marekani huku akikimbiza vibaya na rekodi yake mojawapo, ijulikanayo kwa jina la All I have, akimshirikisha mmoja wa wanamuziki wa R&B paris  mpango mzima waweza tembelea pia wavuti yake, www.ardokingmusic.com.
“Kiukweli Deo, Mungu anasaidia, mambo yanakwenda vyema, tangu tumeachana kitambo kile hapa Mwanza tukiwa pamoja katika harakati zile za maisha, mambo mperampera hivi sasa.”Alisema Ardoking Simple wakati akizungumza nami, katika Hotel ya Mwanza Institute, Jijini Mwanza, tukila bata kwa pamoja, mara baada ya kudondoka kutoka unyamwezini hivi karibuni.