Saturday 1 March 2014

MASHINDANO YA SOKA LA VIJANA TANZANIA YAANZA MWANZA, JUMLA YA TIMU 12 KUTOKA MIKOA YA TANZANIA BARA YASHIRIKI KATIKA MASHINDANO HAYO.


Mashindano ya soka ya vijana nchini Tanzania yaanza Mwanza hapo jana huku yakishirikisha ujmla ya mikoa 12 ya Tanzania bara. 

 Mashindano hayo yameandaliwa na Alliane school academy ya Mwanza huku yakifunguliwa na Ayoub Nyenzi, mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana kutoka shilikisho la soka nchini Tanzania TFF.

Katika mchezo wa ufunguzi wenyeji Alliance walianza vyema baada ya kuwafunga timu ya Future kutoka Arusha mabao 2 - 1 katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Jijini Mwanza.

Akifungua mashindano hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka, mwenyekiti wa kamati ya soka loa vijana kutoka TFF, Ayoub Nyenzi amesema kuwa litayaweka katika kalenda yake mashindano hayo ili kuyaongezea hamasa mashindano hayo, yenye lengo la kuibua vipaji vya soka kwa vijana nchini Tanzania.

Nyenzi aliwataka vijana kuondokana na tabia ya utumiaji mihadarati kama kweli wanataka kuliendeleza soka lao.

Mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana kutoka TFF, Ayoub Nyenzi wakati akifungua mashindano ya soka la vijana kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

 Timu shiriki zikishiriki katika mandamano ya mashindano hayo yaliyoanzia kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana kuelekea CCM Kirumba, ijumaa iliyopita.