Wednesday 13 November 2013

WAAMUZI WATAKAOCHEZESHA KOMBE LA CHALENJI WAJULIKANA



Nicholas Musonye, katibu mkuu wa CECAFA.

CECAFA laweka hadharani majina ya waamuzi na wasaidizi wao watakaochezesha kombe la Chalenji mwaka huu huko Nairobi.

                                       
                                            Na. Mwandishi wetu.


Baraza la soka kwa nchi za ukanda wa Afrika mashariki na kati CECAFA, jumatatu iliyopita limeweka hadharani majina 18 ya waamuzi wa mchezo wa soka watakaosafiri hadi jijini Nairobi nchini Kenya, kwa ajili ya mashindano ya kombe La Chalenji yanayotarajia kuanza kurindima hapo novemba 27 mwaka huu.

Majina hayo 18 ya waamuzi watakaochezesha katika mechi za mashindano hayo huko Nairobi, yametangazwa na katibu mkuu wa CECAFA, Nicholas Msonye.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CECAFA, kupitia ofisa habari wake Rogers Mulindwa, na nakala yake kukifikia Kisima hiki cha habari, imeeleza kuwa waamuzi watakuwa tisa pamoja na wasaidizi tisa na kwamba waamuzi hao watafanya mtihani kwa vitendo yaani copatest pamoja na kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kufunguliwa kwa pazia la mashindano hayo.


Majina ya waamuzi wa kati ni kama ifuatavyo.
1.    Anthony Okwayo-Kenya
2.    Denis Batte-Uganda
3.    Wish Yabarow- Somalia
4.    Israel Mujuni- Tanzania
5.    Louis Hakizimana- Rwanda
6.    ThieryNkurunziza- Burundi
7.    WaziriSheha- Zanzibar
8.    GebremichaelLuleseged- Eritrea
9.    KheiralaMurtaz - Sudan
Waamuzi wasaidizi majina yao ni kama ifuatavyo.
1.    Gilbert Cheruiyot- Kenya
2.    TonnyKidiya- Kenya
3.    Mark sonko- Uganda
4.    FedinardChacha- Tanzania
5.    Suleiman Bashir- Somalia
6.    Fraser Zakara-South Sudan
7.    SimbaHonore-Rwanda
8.    Hamid Idam- Sudan
9.    KinfeYimla-Ethiopia