Thursday 26 December 2013

TANZANIA YATAKIWA KUFANYIWA UPONYAJI, MAKAMBA.>>>>>>>>>



Naibu Waziri wa Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano, Januari Makamba akizungumza na Maskofu na Wachungaji wa Umojawa Makanisa ya Kikristo Jijini Mwanza jana.Kulia ni Katibu wa Umoj huo, Askofu Alex Mwakisumbwa ,wa plpilini Mwenyekiti wa Umoja huo, Askofu Charles Sekelwa na wa kwanza kushoto ni Mratibu wa Tamasgha la Krisimas Fabian Fanuel na wa pili ni Askofu Zenobius Isaya Makamu mwenyekiti wa Umoja huo wa makanisa .




Tanzania yahitaji maombi ya uponyaji ya hali ya juu kutokana na mgawanyiko wa watu wachache walio na uroho wa kujinufaisha na rasilimali za nchi.
Na. Baltazar Mashaka.
                   
NAIBU Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Januari Makamba, amesema Tanzania kama Taifa,linahitaji uponyaji wa hali juu kutokana mgawanyiko wa watu wachache kujinufaisha na rasilimali za nchi badala ya wengi .

Alisema katika uponyaji huo wa kizazi cha sasa Viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa  ingaa wanafanya kazi katika mazingira magumu kutokana na shughuli yao kuingiliwa na matapeli kama ilivyo shughuli ya siasa.

Kwamba Watanzania tumejaribiwa katika umoja wetu kwa sababu ya changamoto ya nyufa zinazotukabili, alizozitaja mwaka  1995, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K.Nyerere,hivyo nchi inapita katika kipindi tete na kigumu .

Makamba alitoa kauli hiyo jana, wakati akizungumza na Maaskofu na Wachungaji wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo Jijini,kwenye chakula cha usiku baada ya tamasha la Krisimasi ambalo alikuwa mgeni rasmi.

“Nataka tuzungumze masuala ya nchi yetu na  sote ni Watanzania,sote tuna hamu ya kufahamu kutafakari  hatma ya nchi yetu,umoja wetu,upendo,amani yetu na utulivu wetu.Nimeamua niseme hay sababu humu ndani kuna watu wazito,Maaskofu na wachungaji a,mbao mnaaminiwa  na kuheshimiwa kwenye jamii kama sisi viongozi wa kisiasa ,lakini kupata kutoka kwenu yale muhimu katika kuendelea kuitengeneza nchi yetu”alisema

Alisema tunapita katika  kipindi tete kidogo katika taifa hili na tunajaribiwa katika umoja  wetu kutokana na mambo yanayoendelea na yaliyowahi kujitokeza huko mkoani  Geita.

 
Mwenyekiti wa Umoja wa Maaknisa ya Kikristo Jijini Mwanaza, Askofu Charles Sekelwa, akimkaribisha Naibu Wziri wa Sayansi,Teknolojia na Mawasiliano, Januar Makamba kabla ya kuzungumza na maaskofu na wachungaji wa umoja wa makanisa hayo jana.

“Mtakumbuka  hotuba ya Mwalimu Nyerere ya Machi  mwaka 1995,alipozungumzia nyufa zinazolikabili taifa ltu,ambazo m ni rushwa, ukabila,udini,uzanzibari na Uzanzibara na akaonya busara iliyotufanya taifa letu liweze kusimama.Kuruhusu nyufa hizo ziendelee,sisi tutakuwa waathirika wa kwanza ana tutalivunja taifa letu  vipande vipande,” alisema Makamba.

Pia akatika hotuba hiy Mwalimu aliasa tuzizibe nyufa hizo ,tuendelee kushikilia mingi ya taifa letu lenye amani,umoja wetu na watu wanaopendana na,ujumbe ambao ni sahihi na umedumu kwa miaka 20 .
  “Nataka niwapongeze sana viongozi wa dini kwav kazi kubwa sana lica ya chokochoko ambapo zipo ma zinazotokea na nyufa hizi zinazoanza kuonekana lakini mmekuwa mkihubiri amani ,upendo,na uvumilivu.Bila mahubiri hayo na bila kazi hiyo mnayoifnya tungekuwa tuko pabaya zaidi kuliko sasa,”alisema Makamba.

Aliwapongeza na kuwahimiza Maaskofu na wachungaji kuendelea hayo kwa kuhubiri amani ,upendo na uvumilivu,licha ya  changamoto ya rushwa,ukabila, ukanda,udini Utanganyika na Uzanzibari.Kwaki kuruhusu nyufa hizo kutalivunja taifa na tutakuwa waathirika wakubwa.

“Sasa taifa letu lina miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika na mwakani tunazmisha mika 50 ya Uhuru wa Zanzibar.Miaka 50 ni mingi kwa binadamu ,kazi ya kulijenga taifa letu ndiyo inaanza.Tunazo changamoto,tunzoweza kuziita za kidunia na za kibidamu za afya,maji na elimu.”

“Lakini zina umuhimu mkubwa na ndizo zinazojenga aidha usawa baina yetu  na kma baadhi wanapata huduma nyingi kuliko wengine na kwa ukubwa kuliko wengine maana yake ni kwamba tunagawanyika ingawaa miganwanyiko hiyo si ya kidini,rangi na kikabil,hapana,iko ya namna gani watu wachache wananufika na keki  (rasilimali) ya taifa kuliko wengine”.

“Sasa serikali hili kwetu ni muhimu sana .Kwamba uongozi wa taifa tunaotarajia kujenga na hakuna kitu muhimu kuendelea kujemga umoja wetu wa taifa letu .Migawanyiko hii ndiyo changamoto ya elimu.Elimu anayoipata mtoto wangu ndiyo anaipata mtoto wa  Rwamgasa,Kwimba na Nyarugusu,Kkwa kizungu wanaita (In Quality) Ikiwa ni pamoja na huduma ya afa anayopta mtu wa mjini aipate na wa kijijini.Hapa ndipo tutapata taifa lenye watu sawa ,leye amani na umoja.”

Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, alisema changamoto zingine ambazo serikali inakabiliana nazo kwenye jamii ni rushwa,ubadhirifu,maovu,wizi wa mali ya umma,ubakaji,utapeli na kuporomoka kwa maadili.Mambo ambayo  viongozi wa dini wanayaona kila siku kwenye jamii  na mengi yanayoonekana na kutokea kila ni kuongezeka kwa maovu.

“Utapeli umezidi, uongo, ubakaji,utapeli,ulaghai,wizi,mauaji.Sasa nini kinaendelea na nini kitatokea.Kwa nini maobu yanaongezeka.Ninyi mnafahamu kuna kipindi  Mungu akikasirika anatoa adhabu.Si kulikuwa na gharika huko nyuma, Sodoma na Gomora,yote hiyo ilikuwa ni dhambi sababu ya watu kumsahamu Mungu.Alitoa adhabu ya maji na kisha moto, sasa adhabu inayofuaata itakuwa ni ipi.Watu wamemsahau Mungu na kupitiliza katika maovu,lakini hatutegemei kufika huko”. Alisema Makamba

Kwamba kama kizazi cha vijana sasa kama kinahitaji uponyaji  na nchi inahitaji uponyaji wa hali ya juu na katika uponyaji huo,viongozi

Dini (Maaskofu na wachungaji ) anaamini pamoja na kufanya kazi katika mazingira magumu sababu ya shughuli zao kuingiliwa na matapeli, kama ilivyo kwa wanasiasa ambao pia wameingiliwa na matapeli.

Alidai kuwa  tunapotafuta uponyaji wan chi yetu Maaskofu na Wachungaji wana nafasi kubwa kwa vile uponyajin unozungumziwa ni  wa maovu ya kiroho,huku Serikali ikiwa na nafasi ya kuadhibu kisheria kwa baadhi ya mambo, hivyo ni vema kushikirikiana ili nchi yetu ipone.

Aidha alidai kuwa viongozi wa kisiasa lazima wawe wasafi jambo ambalo ni muhimu sana,kama ilivyo kwa Maaskofu wanapohubiri watu waache maovu  lazima wawe wasafi, na akatoa mfano wa mama mmoja aliyemepeleka mwanaye kwa Khalifa sababu ya kuiba kulamba sukari kila siku.

“Anayesema unalamba sukari mtazame je, ana ania ya kulamba pia ? Tunapo kuja kuomba uongozi zipo sifa,wapo wanaokuja kanisani.Kuongoza watu wa Mungu ni kazi,ni mamlaka kubwa sana, na  tunao… na vigezo lazima viwe vikubwa sana ”alisema Huku akinuu kifungu cha Biblia kaka kitabu cha Yeremia 1:7

“Bwana akaniambia, usiseme mimi ni mtoto, utakwenda kwa kila mtu na utamwambia…..,Akanigusa akanitia mafuta…na kusema nimekuweka juu ya mataifa ,kubomoa,kuangamiza, kujenga na kupanda.Kazi mliyopewa ni kubomoa, kuharibu na kuiponya nchi yetu,hivyo nawasihi huko mbele wakijitokeza vijana uongozi huo kautoa Mungu.Yeremia si pekee yake wapo wengi,”alisema Makamba

Naibu Waziri huyo alisisitiza kuwa anawapa matumaini viongozi hao wa dini kufanya jithada zaa kuponya kizazi kipya cha uongozi usio na makandokando na kuomba wakiunge mkono wakijitokeza kuomba uongozi wa nchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa hayo ya Kikristo,Askofu  Charles Sekelwa alisema , kauli na maneno ya Makamba siku zote wamekuwa wakiomba kupata kiongozi sahihi atakayesimamia kanisa na taifa na si kanisa tu lakini pia Mungu anatumia vijana makini  na wazee wanatupwa. 

“Tusiogope kukutana na watu wote ila Mungu atupe hekima ya kutambua sifa ya kiongozi.Tunahitaji kiongozi wa kulikomboa taifa hili.Sote ni mashahidi lakini sitaki kuukosoa uongozi uliopo madarakani,”alisema na kuongeza;

“Viongozi wa dini tukubaliane kuwa walezi na tusimkatae mtu kwa dini yake wala kabila yake.Wakijitookeza vjana huko mbele tuwaunge mkono, hayo mameno ni ya mtu mwenye hekima.Tunaongozwa na kiroho na ninyi ni kwa kaisari na wanasiasa wasijione wao ni wakubwa kuliko wa Kiroho.”

MANCHESTER UNITED YASHEREHEKEA VIZURI BOXING DAY.>>>>>>>>>



Ligi kuu ya soka ya England.
·    Mashetani wekundu wawararua  Hull  3 - 2
·    Sasa wafikisha pointi 31 kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Na. Deo Kaji Makomba.

Timu ya mashetani wekundu wa Englang, Manchester United, ikiwa nyuma, imeweza kusawazisha mabao mawili na hatimaye  kupata la tatu na hivyo  kuweza kuibuka na ushindi wa mabao 3 – 2 ugenini dhidi ya Hull City, katika moja ya mchezo wa hekaheka za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya soka ya England, uliochezwa mapema siku hii ya Boxing day.

Hull ndio walikuwa wa kwanza kulisabahi lango la Mashetani hao wekundu, katika dakika ya 4 ya mchezo kupitia kwa James Chester, mlinzi wa zamani wa Manchester United.
Hull City ikicheza nyumbani, iliongeza bao la pili wakati huu likifungwa na David Meyler, aliyeachia mkwaju mkali ambao ulimpalaza Jonny Evans na kisha kutumbukia wavuni.

Lakini Manchester United wakitokea nyuma kwa kutumia miongoni mwa silaha yake Rooney,  aliyepiga mpira wa adhabu kwa uhakika na kumkuta  Chris Smalling aliyekwamisha bao la kwanza kwa Mashetani hao wekundu wa England kunako dakika ya 19 ya mchezo na muda mfupi badae Rooney akaandika bao la pili kunako dakika ya 26.

James Chester wa Hull City alijifunga goli wakati wa harakati za kuondosha hatari langoni mwake na hivyo kusababisha Manchester United kujipatia bao la tatu kunako dakika ya 66.

Na hadi mchezo unamalizika Manchester wameibuka na ushindi wa magoli 3 – 1, dhidi ya wenyeji Hull na hivyo kufikishia pointi 31 kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka ya England hivi sasa.

ALLAN CUURBISHLEY, BOSI MPYA FULHAM.

Allan Curbishley, Bosi mpya wa timu ya soka ya Fulham ya England.







Curbishley: Bosi wa zamani wa West Ham na Charlton ajiunga na Fulham.

Na. Deo Kaji Makomba.

Nchini England, Alan Curbishley ameteuliwa kuwa mkurugenzi katika benchi la ufundi kwenye klabu ya soka ya Fulham iliyoko ligi kuu soka ya England inayoendelea kutimka vumbi hivi sasa. 

 Alan ambaye pia aliwahi kuwa bosi wa klabu ya soka ya Charlton, amerejea zaidi ya mara tano katika klabu ya soka baada ya kuiacha West Ham.

Alan mwenye umri wa miaka 56, mara baada ya kuelezwa atakuwa meneja ajaye wa timu ya taifa ya England, ameunganisha nguvu zake na Rene Meulenteen, ambaye alichukuwa mikoba ya Martin Jol kama meneja wa klabu hiyo, mapema mwezi huu.

“Alan anayo rekodi nzuri na anaelewa vyema nini atafanya kufikia mafanikio,” alisema Meulensteen.
Fullham, wanaowakabili Norwich kwenye uwanja wa Carrow Road siku hii ya Boxing day, hivi sasa wako katika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi kuu soka ya England inayoendelea kuchanja mbuga hivi sasa.




UFUATAO NI MSIMAMO WA LIGI KUU YA SOKA YA ENGLAND HADI  HIVI SASA, KABLA YA MECHI ZA LEO MCHANA.

Position
Team
Played
Goal Difference
Points


1
17
23
36
2
17
16
36
3
17
31
35
4
17
14
34
5
17
13
34
6
17
2
30
7
17
-5
30
8
17
8
28
9
17
4
24
10
17
-4
21
11
17
0
20
12
17
-6
20
13
17
-6
19
14
17
-14
19
15
17
-12
17
16
17
-5
16
17
17
-8
14
18
17
-16
13
19
17
-17
13
20
17
-18
10