Thursday 26 December 2013

MANCHESTER UNITED YASHEREHEKEA VIZURI BOXING DAY.>>>>>>>>>



Ligi kuu ya soka ya England.
·    Mashetani wekundu wawararua  Hull  3 - 2
·    Sasa wafikisha pointi 31 kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Na. Deo Kaji Makomba.

Timu ya mashetani wekundu wa Englang, Manchester United, ikiwa nyuma, imeweza kusawazisha mabao mawili na hatimaye  kupata la tatu na hivyo  kuweza kuibuka na ushindi wa mabao 3 – 2 ugenini dhidi ya Hull City, katika moja ya mchezo wa hekaheka za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya soka ya England, uliochezwa mapema siku hii ya Boxing day.

Hull ndio walikuwa wa kwanza kulisabahi lango la Mashetani hao wekundu, katika dakika ya 4 ya mchezo kupitia kwa James Chester, mlinzi wa zamani wa Manchester United.
Hull City ikicheza nyumbani, iliongeza bao la pili wakati huu likifungwa na David Meyler, aliyeachia mkwaju mkali ambao ulimpalaza Jonny Evans na kisha kutumbukia wavuni.

Lakini Manchester United wakitokea nyuma kwa kutumia miongoni mwa silaha yake Rooney,  aliyepiga mpira wa adhabu kwa uhakika na kumkuta  Chris Smalling aliyekwamisha bao la kwanza kwa Mashetani hao wekundu wa England kunako dakika ya 19 ya mchezo na muda mfupi badae Rooney akaandika bao la pili kunako dakika ya 26.

James Chester wa Hull City alijifunga goli wakati wa harakati za kuondosha hatari langoni mwake na hivyo kusababisha Manchester United kujipatia bao la tatu kunako dakika ya 66.

Na hadi mchezo unamalizika Manchester wameibuka na ushindi wa magoli 3 – 1, dhidi ya wenyeji Hull na hivyo kufikishia pointi 31 kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka ya England hivi sasa.

No comments:

Post a Comment