Monday 23 September 2013

KAMPUNI YA MAFUTA NCHINI TANZANIA, KUUZA MAFUTA NCHI NZIMA.

 Mmoja wa wakurugenzi wa East Africa Fossil company Limited, Bw. Steven Marwa Mathayo akizungumza katika promotion ya kampuni yake iliyofanyika jumapili iliyopita jijini Mwanza.

Kampuni ya uingizaji na uuzaji mafuta nchini Tanzania ya EAFCON yakusudia kuuza mafuta katika mikoa yote ya Tanzania.

  •      Kutoa ajira ya zaidi ya watu 1,000

  •      Yaendesha promotion kwa wateja wake jijini Mwanza

  •      Ni kampuni ya kizalendo yenye makao yake makuu mjini Musoma mkoani Mara.    

                                       Na. deo kaji makomba.

Katika kuhakikisha idadi kubwa ya watanzania wanapata huduma iliyo bora ya nishati ya mafuta, kampuni ya kizalendo ya  East Africa fosill , EAFCO , imesema kuwa hivi sasa iko katika mpango wa kuhakikisha inapeleka huduma ya bidhaa hiyo katika mikoa yote ya Tanzania.


Kauli hiyo imetolewa na mmoja wa wakurugenzi wa EAFCO, Bw. Steven Marwa  Mathayo wakati akizungumza katika kilele cha promotion iliyoendeshwa na kampuni hiyo, ya weka mafuta katika vituo vyake vilivyopo jijini Mwanza.


Akizungumza wakati wa utoaji wa zawadi kwa washindi mbalimbali wa promotion ya weka mafuta katika vituo vya mafuta vya EAFCO,  Bw. Mathayo alisema ni lengo la kampuni yake kuhakikisha inasambaza huduma ya nishati hiyo nchi zima.
 Mkurugenzi wa EAFCO Bw. Steven Marwa Matayo, akikabidhi zawadi ya friji kwa mmoja wa washindi wa promotion iliyoendeshwa na kampuni yake ya uuzaji mafuta nchini Tanzania, kwa Bw. Mwinyi Rajabu mshindi wa zawadi kubwa ya pikipiki.

Bw. Mathayo alisema kuwa licha ya lengo la kampuni yake hiyo ya kizalendo kusambaza huduma ya nishati ya mafuta ili kutoa huduma hiyo kwa watanzania, lakini kampuni yake imelenga pia kutoa ajira kwa vijana wengi wa kitanzania na lengo likiwa ni kuajiri zaidi ya wafanyakazi 1,000 na hadi hivi sasa tayari  zaidi ya watanzania 200 wameajiliwa na kampuni hiyo.


Aidha Bw. Mathayo ameongeza kuwa hadi hivi sasa kampuni yake inatoa huduma kwa mikoa mitano ya Tanzania na tayari hivi sasa kampuni yake imejitanua pia na kuuza bidhaa hiyo ya nishati ya mafuta hadi nchi za nje ikiwemo Rwanda na Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo.



 Burudani nayo haikuwa nyuma, hapa kikundi cha burudani kikifanya vitu vyake, wakati ya promotion, ya wateja wanaonywesha mafuta katika vituo vya mafuta vinavyomilikiwa na kampuni ya kizalendo ya EAFCO, jumapili iliyopita.
“ Kiukweli kampuni yetu ni ya kizalendo kabisa. Tulianza na kituo kimoja cha uuzaji mafuta, lakini sasa tunaingiza mafuta kutoka nje na kuyauza kwa wateja wetu  katika ubora wa hali ya juu.” Alisema Mathayo mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya EAFCO  yenye makao makuu yake mjini Musoma mkoani Mara.

Naye kwa upande wake meneja masoko na mauzo, Bw. Castor Masabo, akizungumzia promotion iliyoendeshwa na kampuni yake ya EAFCO, alisema kuwa promotion hiyo ililenga kuwaonesha wateja wake kuwa inawajali nahivyo kurejesha fadhira kwa jamii.


Bw. Masabo alisema kuwa promotion hizo katika kampuni yake zitakuwa endelevu zikilenga katika kutoa  huduma kwa jamii, ikiwemo masuala ya elimu pamoja na afya.
 Meneja masoko na mauzo, Bw. Castro Masabo, akizungumza na wandishi wa habari kuhusiana na promotion iliyoendeshwa na kampuni yake ya EAFCO, jijini Mwanza.


Wateja mbalimbali wanatumia huduma ya nishati ya mafuta inayotolewa na kampuni ya East Africa Fossil, EAFCO, walijinyakulia zawadi mbalimbali katika promotion iliyoendeshwa na kampuni yake jumapili iliyopita katika viwanja vya moja kituo cha kampuni hiyo cha Jambo Filling Station, kilichopo maeneo ya mlango mmoja jijini Mwanza.


Bw. Mwinyi Rajabu Silabu, aliibuka mshindi wa zawadi kubwa ya pikipiki, friji, saa za ukutani, huku mfungaji bora wa ligi kuu soka ya safari lager mnamo mwaka 1997, Elias Mwachura, naye akijinyakulia zawadi lukuki katika promotion hiyo.

Picha na matukio yote katika promotion ya weka mafuta na vituo vya EAFCO vilivyoko jijini Mwanza hapa chini.( Picha zote na Martin Jonas Kimbavala, wa Kisima cha habari )




 Umati wa watu wakishuhudia promotion iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni ya uuzaji mafuta nchini Tanzania, EAFCO, jijini Mwanza.

 Elias Mwachura, mfungaji bora wa ligi kuu ya soka ya safari lager mnamo mwaka 1997, akikabidhiwa zawadi katika promotion hiyo


Kutoka kushoto ni mmoja wa wakurugenzi wa EAFCO Bw. Steven Marwa, akifuatiwa na Mwinyi Rajabu wa Pasiansi, alijishindia zawadi ya pikipiki, na aliye na miwani kichwani ni Castro Masabo, meneja masoko na mauzo EAFCO.

No comments:

Post a Comment