Saturday 22 June 2013

KATIKA SOKA HUKO MAJUU




LIVERPOOL YAMSAINISHA ALIYEKUWA MSHAMBULIAJI WA SEVILLA NA KIKOSI CHA UNDER- 21 CHA HISPANIA.


·        Ni katika mandalizi ya kimuhemuhe cha ligi kuu ya England.

·         Kuungana na Simon Mignolet.


Na. Deo Kaji Makomba

Barani ulaya klabu ya kandanda ya Liverpool ya nchini Englang, imemsajili mshambuliaji wa timu ya Sevilla, Luis Alberto kwa mkataba wa muda murefu, kwa dau linaloaminika kuwa paundi milioni 6.8

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20, alikuwa akichezea kwa mkopo katika kikosi B cha klabu ya soka ya Barcelona ya nchini Uispania, lakini mabingwa hao wa Uispania wakaamua kuchukua maamuzi ya kuwaruhusu Liverpool kumsajili mchezaji huyo ambaye pia anachezea kikosi cha Uispania kwa wachezaji walio chini ya umri wa miaka 21.

“Ana wasifu uliokamilika kimpira na anatufaa kuwa mchezaji wa Liverpool.” Amesema bosi wa wekundu hao, Brendan Rodgers.

“ Ninatizama mbele kufanya kazi nay eye kwa ajili ya kuendeleza kipaji chake.” Aliongeza kuema bosi huyo.
 Alberto alijiunga na klabu ya Sevilla akiwa na umri wa miaka 18 hapo mwezi April mwaka 2011.

Mchezaji huyo wa zamani katika kikosi cha umri chini ya miaka 18 na chini ya miaka 19 amecheza mechi 38 katika kikosi B cha Barcelona msimu uliopita, huku akipachika wavuni magoli 17.

Atakwenda kuungana Anfield na Simon Mignolet,na mlindamlango anayetarajiwa kukamilisha dili ya paund million 9 wiki ijayo kwa ajili ya kuidakia timu hiyo katika msimu mpya wa ligi kuu ya soka ya England.

LIVER WAFANYA MIPANGO KUMSAJIRI KIPA WA SUNDERLAND


·         Ni Simon Mignolet
                
Na. Deo Kaji Makomba

Barani ulaya uongozi wa majongoo wa London timu ya Liverpool wako katika mpango wa kumsajili mlinda mlango wa timu ya soka ya Sunderland, Simon Mignolet kwa dau la paundi milioni tisa, mchakato mzima ukitarajiwa kufanyika wiki ijayo. 
Habari hii kwa kina inaendelea katika ukurasa wa Sports.>>>>>>>>>