Tuesday 3 December 2013

CHADEMA ILEMELA YAKANUSHA MATAMKO YA KUWAPIGA MARUFUKU MBOWE NA SLAA KUKANYAGA MWANZA.

Mwenyekiti wa chama chama cha Demokrasia na maendeleo, CHADEMA, wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Bw. Yunisi A Chilongozi.

Uongozi CHADEMA  wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, wakanusha tamko lililotolewa na wanaojiita sauti ya viajana wa CHADEMA la kuwapiga marufuku Kina Slaa Mbowe kukanyaga Mwanza

·    Wasema ni kikundi cha wahuni kilichotoa tamko hilo.
·    Mwenyekiti wa CHADEMA Singida naye ajiuzulu nafasi hiyo.

                                                     Na. Deo Kaji Makomba.

Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, kimekanusha vikali taarifa zilizotolewa hivi karibuni katika vyombo mbalimbali vya habari kuwa, uongozi wa sauti ya vijana wa CHADEMA, mkoani Mwanza, unawazuia  viongozi wa chama hicho kitaifa kutokufika maeneo ya Mwanza  kwa madai kuwa, hawaridhishwi na sababu zilizowavua uongozi baadhi ya wana CHADEMA, akiwemo Zuberi  Zitto Kabwe.

Kauli hiyo ya CHADEMA wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza imetolewa na uongozi wa chama hicho ngazi hiyo ya wilaya, baada ya Bw. Robert  E. Gwancele, aliyejitamburisha kama mwenyekiti wa sauti  ya vijana ya CHADEMA mkoani Mwanza, kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa wana CHADEMA Mwanza, hawatataka kuwaona maeneo ya Mwanza na mwenyekiti wa taifa wa chama hicho Wilbroad Silaa pamoja na katibu wake Freeman Mbowe.

Akizungumza katika mkutano na wandishi wa habari kwenye hotel ya Lenana iliyopo Pasiansi jijini Mwanza, mwenyekiti wa CHADEMA, wilaya ya Ilemela, Bw. Yunisi A. Chilongozi, amesema kuwa chama wilaya yake inaunga mkono maamuzi yaliyochukuliwa na kamati kuu ya utendaji ya chama hicho taifa ya kuwavua madaraka Zito Zuberi Kabwe na wenzake na kuwaomba wanachama wa CHADEMA kuyapuuza matamko yaliyotolewa na kikundi walichokiita ni cha kihuni kinachoendeshwa na Bw. Gwanchele.

Aidha Bw. Chilongozi ameongeza kusema kuwa kikundi hicho kinachowapiga marufuku viongozi wa CHADEMA taifa kutofika Mwanza hawana mamlaka yoyote na kwamba Chama hicho ngazi ya wilaya ya Ilemela kinamchukulia hatua kali Bw. Gwanchele ambaye ni mwanachama wa kawaida ndani ya chama hicho.

Bw. Chilongozi alienda mbali kwa kusema kuwa chama chake ni makini na ndiyo maana kimekuwa kikiwaadhibu viongozi na wanachama wake ambao huleta mbinu za kukisaliti chama kwa kutumiwa na wapinzani wao chama cha Mapinduzi, CCM.

Lakini wakati hayo yakitokea, hali inazidi kuonekana kuwa  si shwari ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo, CHADEMA, kufuatia mwenyekiti wa chama hicho mkoani  Singida kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo.

Wakati huohuo habari kutoka Arusha zilieleza kuwa, ofisi ya CHADEMA, jijini iliungua moto  jumanne hii majira ya saa 12 asubuhi, baada ya mlinzi wa ofisi hiyo kuwa ameondoka kwenye eneo lake la ulinzi.
Polisi mkoani Arusha, inaendesha uchunguzi ili kuweza kubaini chanzo cha moto huo.

ASHA ROSE MIGIRO ATEULIWA NA RAIS KUWA MBUNGE.

Aliyewahi kuwa katibu mkuu msaidizi wa Umoja wa mataifa, UN, Asha Rose Migiro, ambaye hivi sasa ameteuliwa kuwa mbunge kupitia CCM.

Nafasi za kuteuliwa za ubunge.
·    Rais amteua Asha Rose Migiro.
·    Uteuzi  huo umeanza tangu jumatatu Desemba 2, 2013.

TAARIFA KUTOKA IKULU.

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dr. Asha Rose Migiro kuwa Mbunge.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es salaamjumanne hii ya Desemba  3, 2013, na katibu mkuu kiongozi, Dr. Florens Turuka imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza tangu jumatatu ya Desemba 2, 2013.

Dr. Asha Rose Migiro, ni katibu wa halmashauri kuu ya taifa, idara ya siasa na uhusiano wa kimataifa katika chama cha Mapinduzi, CCM.