Sunday 7 July 2013

MAMBO YALIVYOKUWA SIKU YA UZINDUZI WA AWALI WA KISIMA CHA HABARI












 Wasomi kutoka chuo cha biashara cha CBE Campus ya Mwanza, wakipata maakuli siku ya uzinduzi wa awali wa Kisima cha habari, jumamosi iliyopita Nyakato National Jijini mwanza.

UZINDUZI WA AWALI WA MTANDAO HUU




VIJANA WANAOMALIZA MASOMO YAO KATIKA VYUO MBALIMBALI TANZANIA WATAKIWA KUFUNGUKA.

·         Ni kiakili zaidi zaidi.

Na. Mwandishi wetu.

 

Vijana wametakiwa kuwa na mawazo ya kufanya kazi za kujiajili hususani wanapokuwa wanamaliza masomo yao, katika vyuo mbalimbali nchini Tanzania, badala ya kuwa na mawazo ya kuajiliwa pindi wamalizapo masomo yao katika Nyanja tofauti.

Kulalamika  na kutokuwa na mawazo ya kusimama mwenyewe  kwa kijana msomi aliyemaliza shahada au sitashahada ya taaluma Fulani, yaelezwa kuwa ni moja ya sumu kali ambayo inadidimiza kwa kiasi kikubwa harakati za kijana huyo kuweza kujikomboa katika suala zima la umasikini.

Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa kampuni BESTCOM, inayojishughulisha na shughuli za utengenezaji milango katika ofisi na mahotel makubwa, nchini, bwana Martin Kimbavala, wakati akizungumza na baadhi ya wanachuo wa mwaka wa mwisho katika chuo cha biashara, CBE, Campus ya Mwanza kutoka katika vitivyo tofauti, kwenye  sherehe fupi ya uzinduzi wa awali wa mtandao huu wa kijamii, kisima cha habari, zilizofanyika jumamosi iliyopita Nyakato National, Jijini Mwanza.

Akizungumza katika sherehe hiyo iliyoambatana na burudani mbalimbali ikiwemo ya muziki, bwana kimbavala ambaye pia ni kijana, amesema kuwa kumekuwa na kasumba ya ajabu kwa baadhi ya vijana wanaomaliza vyuo tofauti  hapa nchini, kuwa na mawazo ya kuajiliwa pindi wamalizapo masomo yao vyuoni, badala ya kuwa na mawazo ya ni jinsi gani wanaweza kufanikiwa na kuondokana na umasikini kwa kutumia fursa zinazowazunguka.

Bwana Kimbavala ameongeza kusema kuwa kwa kutumia fursa zilizopo na kutengeneza umoja wao, wanaweza kuyafanya mawazo yao kuwa bidhaa inayohitajika sokoni na hatimaye kuiuuza.

Deokajimakomba.blogspot.com ama Kisima cha habari ni mtandao wa kijamii, ulioanzishwa na vijana wawili ambao wanakamilisha masomo yao ya stashahada ya masoko katika chuo cha biashara CBE, Campus ya Mwanza.

Mtandao huu wa kijamii, umeanzishwa takribani mwezi sasa umepita lengo kubwa ikiwa ni kutafuta habari zilizosahihi katika jamii na kuziandika katika ukurasa huu na wandishi waliobobea  ili kuweza kumpatia fursa yeyote Yule mwenye kumudu kupata huduma ya internet kuweza  kupata habari kemkem bila kusahau michezo na burudani .

Kwa upande wake mkurugenzi wa mtandao huu , bwana Deo Kaji Makomba, akizungumza katika sherehe hiyo fupi, ambayo wadau mbalimbali walipata fursa ya kuhudhuria katika uzinduzi huo wa awali, alisema kuwa, kutokana na kila binadamu kuwanayo haki ya kupata habari sahihi na kwa wakati muafaka,  kama kisima cha habari wameamua kufanya kila wawezalo kuhakikisha kiu ya binadamu kuweza kupata habari inamalizika.

 Mkurugenzi wa mtandao wa kijamii wa habari, kisima cha habari,Deo kaji makomba, akizungumza jambo katika sherehe za uzinduzi wa awali wa kisima cha habari(Picha na maktaba yetu)

“Mawazo yapo ndugu yangu lakini tatizo hapa linaonekana ni mtaji. Sasa kama tatizo ni mtaji unafanya nini sasa ili kuweza kufikia malengo, hapo akili ndio inatakiwa kuchemka na kuanza kuangalia fursa zilizopo ili kuweza kuona tunasonga mbele”. Alisema Makomba.

Katika uzinduzi huo wa awali wa mtandao huu uliofanyika jumamosi iliyopita, ulihudhuriwa na baadhi ya wanachuo wa CBE, Campus ya Mwanza kutoka katika vitivyo tofautitofati ikiwemo kitivyo cha masoko, ugavi na usambazaji pamoja na utawala wa biashara.