Kikosi cha Tanzanite
Tanzanite yaua
huko Maputo.
- Yafuzu kucheza raundi ya pili ya michuano ya kombe la dunia.
- Yawaadhibu wasichana wenzao wa Msumbiji 5 – 1.
- Kutua Dar jumapili hii mchana.
Na. Mwandishi
wetu.
Timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka
20 (Tanzanite) imefuzu kucheza raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Dunia kwa
ushindi wa jumla ya mabao 15-1 baada ya jumamosi hii (Novemba 9 mwaka huu) kuibugiza
Msumbiji mabao 5-1.
Mabao ya Tanzanite katika mechi hiyo
iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto jijini Maputo yalipatikana kupitia kwa
Sherida Boniface alipiga matatu (hat trick) wakati mengine yalifungwa na
Vumilia Maarifa na Donesia Minja.
Msafara wa Tanzanite ulioongozwa na
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Kidao Wilfred utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
kesho Jumapili (Novemba 10 mwaka huu) saa 8.30 mchana kwa ndege ya LAM.
Tanzanite inayofundishwa na Rogasian
Kaijage itacheza mechi ya raundi ya pili dhidi ya Afrika Kusini.
Mechi ya
kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Desemba 6 na 8 mwaka huu wakati
ile ya marudiano itafanyika Afrika Kusini kati ya Desemba 20-22 mwaka huu.