Friday 26 July 2013

HABARI NA MATUKIO MOTOMOTO NDANI YA KISIMA CHA HABARI

Meneja wa biahara wakampuni ya simu Tanzania, TTCL mkoa wa Mwanza bwana Pius Ng'ingo, akieleza jambo mbele ya mkurugenzi wa Kisima cha habari bwana Deo Kaji Makomba, wakati Kisima cha habari kilipotembelea katika ofisi za TTCL mkoa wa Mwanza.


MFUMKO WA UTITIRI WA MITANDAO YA MAWASILIANO NCHINI TANZANIA.   

Watuamiaji wa mitandao hiyo nchini watakiwa kuwa makani

·                     Ni wakati ule wanapofanya maamuzi ya ni mtandandao upi wautumie.

·                    Yaelezwa kwa kutokufanya hivyo watapoteza rasilimali nyinyingi ikiwemo muda.

 Na. deo kaji makomba

Kufuatia kuwepo na utitiri wa mitandao ya mawasiliano, watu wanaotumia mitandao hiyo wametakiwa kuwa makini wakati wanapofanya uchaguzi wa mtandao upi autumie ili kuweza kuondokana na ubabaishaji uliopo katika mitandao mingine hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na meneja mauzo wa kampuni ya simu Tanzania, TTCL mkoani Mwanza, bwana Pius Ng’ingo wakati akizungumza na kisima cha habari ofisini kwake mtaa wa Nyamagana jijini Mwanza.

Amesema kuwa ni ukweli usiopingika kuwa kukuwa kwa teknolojia mahali popote duniani, ni chachu ya kuwepo kwa maendeleo hususani katika nyanja ya mawasiliano, lakini watumiaji pia wa mitandayo hiyo ya mawasiliano wanapaswa kuwa makini na ni mtandao upi wanapaswa kutumia ili kuweza kurahisisha mambo kwa uharaka zaidi ili kuweza kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia katika masuala mazima kiuchumi na kibiashara.
 Bi Rose Nzengula, mtoa huduma kwa wateja wa TTCL mkoa wa Mwanza(Customer care) alipokutwa na kisima cha habari wakati akiwajibika katika kazi

Akitolea mfano amesema kuwa mtandao wa simu wa TTCL ndio mtandao pekee ambao utamfaa mtumiaji hasa kutokana na kampuni yake kuwa na huduma nzuri ikiwemo ya internet.

Amesema kutoka na mambo mengi duniani hivi sasa kutegemea huduma ya internet, mtumiaji ama mteja anapaswa kupata internet iliyo haraka ili aweze kufanya kazi zake barabara.
 Bwana Pius Ng'ingo meneja biashara wa TTCL mkoa wa Mwanza, kulia, akiwa na bwana Michail Mutharis anayeonekana kushoto ambaye ni ofisa wa masuala ya fedha TTCL mkoa wa mwanza

“Bwana Makomba, unajua muda ni rasilimali, sasa mtu kama atatumia muda wa saa anahangaikia kupata mtandao, atakuwa amepoteza mambo mengi, hivyo wakitumia mtandao wa TTCL utawasaidia kwani kasi yake ni nzuri.” Alisema bwana Ng’ingo.
 TTCL mkoa wa Mwanza haiko nyuma kutoa mafunzo kwa vitendo. Hapa anaonekana Bi. Imelda Ngassa mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha SAUT, akipata huduma ya vitendo jini ya kutoa huduma kwa wateja wa TTCL mkoa wa Mwanza.(Picha zote na Charles John wa Kisima cha habari)

Takribani miaka 15 hivi sasa tangu kufunguliwa kwa makampuni mbalimbali ya mitandao ya simu nchini Tanzania kumekuwepo na ushindani huku makampuni hayo yakishindana katika kutoa huduma kwa wateja wake na kuvutia upande wake.