Friday 20 December 2013

MAMBO SI SHWARI HUKO SUDANI YA KUSINI.>>>>>>>>>>>>>>>>

Picha ikionesha hali ya mambo vile ilivyo huko Sudani ya Kusini.

“Kimenuka” Sudani ya Kusini.
·    Hali ya wasiwasi yatanda.
·    Kambi ya Umoja wa mataifa yashambuliwa.
·    Vurugu hizo zawahusisha Vijana wa kabila la Lou Nuer.

Na. Mwandishi wetu.

Hali ni ya wasi wasi huko Sudan Kusini imezidi kutanda miongoni mwa wananchi wan chi hiyo, huku umoja wa mataifa ukieleza ya kuwa  hali katika jimbo la Jonglei imezorota kufuatia shambulio la Alhamisi kwenye kambi ya Umoja wa mataifa huko Akobo ambako wakazi wamepata hifadhi.

Kulingana  na ripoti ya Umoja wa Mataifa  yaeleza ya kuwa  umepoteza mawasiliano na kambi hiyo na inapanga kupeleka ndege hadi Akobo Ijumaa ili kuwaondosha wafanyakazi wake na kuweza kutathimini kilichowafika wakazi waliopewa hifadhi huko.

Yaelezwa kuwa  kundi la vijana kutoka katika  kabila la Lou Nuer waliingia kwa nguvu kambi ya muda ya ofisi ya umoja wa mataifa huko Akobo.

Wakati huo kulikuwepo na walinda amani 43 kutoka India polisi washauri wa Umoja wa mataifa sita na wafanyakzi wawili wa umoja wa mataifa ndani ya kambi, mbali na raia 32 wa kabila la Dinka walopewa hifadhi huko.

Ofisi ya umoja wa mataifa Sudan Kusini UNMISS inaeleza kwamba inapeleka ndege Ijumaa asubuhi ili  kuwaondoa wafanyakazi wa Umoja wa mataifa ambao wako salama katika kambi ya jeshi la ukombozi la Sudan Kusini (SPLA) katika eneo hilo.

Mawasiliano na kambi ya Umoja wa Mataifa yamekatwa na ofisi kuu inataka kujua kilichowafika raia 32  waliokuwepo ndani wakati wa shambulio na walinda amani watatu ambao hawajulikani walipo.

Mbali na hayo walinda amani 60 wanatazamiwa kupelekwa huko Akobo ili kuimarisha kambi.Naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa Jan Eliasson aliwambia waandishi habari kwamba wanachunguza habari zinazoeleza kulikuwepo na watu waliojeruhiwa.

Makamu rais wa zamani wa Sudan Riek Machar aliyefukuzwa na rais Salva Kiir ni kutoka kabila la Lou Nuer, huku  Rais Kiir mdinka amemtuhumu Machar na wafuasi wake kwa kujaribu kupanga mapinduzi dhidi ya serikali yake mapema wiki hii na hivyo kuzusha ghasia  ambazo maafisa wanasema zimesababisha vifo vya watu wapatao 500.

Bw Eliasson amehimiza pande zote mbili kuanza mazungumzo akisema hiyo ndio njia pekee ya kuzuia ghasia kuzorota.

Wakati huo huo Umoja wa Mataifa unaeleza kwamba hali huko Juba, ambako ghasia zilizuka Jumapili inaonekana kuwa tulivu hapo jana hata hivyo watu wangali wanatafuta hifadhi. Umoja wa mataifa una kikosi cha walinda amani 7000  na polisi huko Sudan kusini ambao jukumu lao miongoni mwa mambo mengine ni kuwalinda raia.