Thursday 24 October 2013

LIGI YA MABINGWA WA SOKA BARANI ULAYA


Ligi ya mabingwa barani Ulaya vipigo vyazidi kutawala.

·    Bayern Munich yaua.
·    Manchester United yaambulia “kamoja tu.”


                               Na. Deo Kaji Makomba.


Huko barani ulaya kivumbi cha ligi soka ya mabingwa barani humo kimezidi kutimka vumbi, huku kukishuhudiwa vigogo kadhaa vya soka barani humo vikishuka katika viwanja tofauti kupepetana.


 klabu ya soka ya Bayern  Munich ya nchini Ujerumani, imezidi kujihakikishia asilimia 100 ya kusonga mbele katika michuano ya ligi ya mabingwa wa soka barani humo kutoka kundi , baada ya kuichakaza timu ya ViKtoria Plzen mabao 5 – 0, katika mchezo uliopigwa usiku wa jana kuamkia leo kwenye uwanja wa Allianz Arena.

Mchezaji Frank Ribery, alifunga magoli mawili timu yake Bayern, bao la kwanza akilifunga kwa njia ya Penaiti kunako dakika ya 25 huku bao lake katika mchezo huo akilifunga katika dakika ya 61 ya mchezo.

David Alaba aliiandikia Bayern bao la pili kunako dakika ya 37 wakati mchezaji Bastian Schweinsteiger akipachika la Nne naye mchezaji Mario Gotze akipigilia msumali wa mwisho katika jeneza la timu ya Viktoria Plzen na katika dakika za mwisho kabla ya mchezo kumalizika na hivyo kuwafanya Bayern Munich wakitoka uwanjani kwa ushindi mnono.

Nayo timu ya mashetani wekundu, Manchester United, wakiwa nyumbani wameweza kuibuka na ushindi wa bao 1 – 0 timu ya Real Sociedad, katika mchezo mwingine wa ligi ya mabingwa wa soka barani ulaya, uliopigwa uiku wa jana kuamkia leo.
 Wachezaji wa United wakifurahia goli lao katika mchezo wao dhidi ya Real Sociedad

Manchester United iliyoko katika nafasi ya Nane katika msimu wa ligi kuu ya soka ya England, walifanikiwa kupata bao hilo baada ya mchezaji Inigo Martine kujifunga mwenyewe wakati akiwa katika hekaheka za kuokoa hatari langoni mwake na kasha kujifunga.

Wakati hayo yakichomoza nao Paris Saint – Germain  wakiwa ugenini, wameweza kuishushia kipigo cha mbwa mwizi cha magoli 5 – 0 timu ya Anderlecht.

Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic amekuwa mchezaji wa kumio kufunga magoli manne katika mechi moja, kwenye michuano hiyo ya ligi ya mabingwa barani ulaya.

Mabao hayo manne ya Ibramovic aliyafunga kunako dakika ya 17, 22, 36 na dakika ya 62 wakati Edinson Kavani akipachika la goli lake katika dakika ya 51 ya mchezo na hivyo timu ya Saint – Germain kuendelea kukalia kigoda katika msimamo kwenye kundi lake.

Nayo Real Madrid ikiwa nyumbani hapo usiku wa jana kuamkia leo, imeweza kuibuka na ushindi wa mabao 2 – 1 dhidi ya vi bibi kizee vya Italia timu ya Juventu Turin.

Mabao ya Real Madrid yalifungwa na Christiano Ronaldo kwa njia ya penaiti kunako dakika ya Nne ya mchezo bao jingine akilifunga kunako dakika ya 29, wakati bao la kufutia machozi kwa upande wa Juve lilipatikana katika dakika ya 22 likufungwa na mchezaji Llorente