Tuesday 6 August 2013

KUELEKEA KIMUHEMUHE CHA LIGI KUU SOKA YA ENGLAND MSIMU HUU



Luis Suarez kuikosa safari ya Liverpool huko Norway kutokana na kuwa majeruhi

 

·        Ni katika mandalizi ya kuelekea kimuhemuhe cha ligi kuu ya soka ya England.

                 

                   Na. deo kaji makomba

Mshambuliaji wa  timu ya soka ya Liver pool ya England, Luis Suarez, ambaye anaonekana kutokutulia,ataikosa ziara ya kimichezo ya kimataifa ya timu yake huko nchini Norway ikiwa ni mandalizi kabla ya kuanza kwa ligi kuu ya soka ya England kutokana na kuwa majeruhi ya mguu.

 Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akiwaniwa na klabu ya Asernal ambayo tayari imekwishatoa ofa mbili ikitaka kumchukua.

Suarez amekwishacheza mechi tatu katika timu yake ya Liver pool dhidi ya Melbourne victory, Thailand na Olmpiakos.

Kwa upande mwingine pilikapilika za usajili wa wachezaji katika msimu wa majira ya kiangazi huko barani ulaya zinazidi kushika kasi huku wachezaji mbalimbali wakitoka katika klabu moja na kusajiliwa na vilabu vingine, kwa  viwango vikubwa vya fedha.

Miongoni mwa wachezaji ambao tayari wamekwishasajiliwa na vilabu tofautitofauti barani humo, ni Edinson Cavan ambaye anatokea FC Napoli na kusaini Paris St Germain ya Ufaransa kwa dau la paun milioni 55, huku mchezaji Falcao akiachana na Atletico Madrid ya Uispania na kudaka mchongo wa kuichezea Monaco ya Ufaransa kwa dau la pauni milioni 50.

 Mchezaji Ednson Cavan ambaye amesajili PSG ya Ufaransa akitokea FC Napoli ya Italia kwa dau la pauni milioni 55


Wachezaji wengine ni Neymar ambaye anatoka Santos kwenda Barcelona kwa dau la pauni milioni 48.6, James Rodriguez kasajiliwa na Monaco ya Ufaransa kwa dau la pauni milioni 38.5 akitokea Porto ya Ureno, wakati mchezaji Frenandinho akitokea Shaktar Donetsk na kujiunga na Manchester City kwa kitita cha pauni milioni 30


WAYNE ROONEY KWENDA CHELSEA AMA KUBAKI MANCHESTER?



Rooney atakiwa kuondoka Manchester, kama kweli ana nia ya kwenda Chelsea. “Paul Ince”
 
Na. deo Kaji Makomba

Huko barani ulaya mshambuliaji wa kimataifa Wayne Rooney anatakiwa kuonesha nia yake kama kweli anataka kuiacha klabu ya Manchester United na kujiunga na Chelsea ya England katika msimu mpya wa ligi kuu ya soka nchini humo.

Ushauri huo umetolewa na mchezaji wa zamani wa mashetani wekundu timu ya Manchester united, Paul Ince.

Manchester United tayari walikwishasema ya kuwa mshambuliaji huyo hauzwi huku wakikataa ofa ya pili kutoka kwa Chelsea yenye thamani ya pauni milioni 25.

“Kama Wayne anataka kuondoka, hiyo ni juu yake kuharakisha mchakato huo.” Alisema Ince ambaye ni meneja wa timu ya Blackpool.

“Lakini Wayne hajaweka hadharani kama anataka kuondoka ama kubakia na United
Itakuwa ni vizuri kujua nini Wayne Roy anataka.”


 Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Mashetani wekundu, Manchester United, Paul Ince.
 
Paul Ince ambaye pia hivi sasa ni bosi wa Blackpool ya England licha ya kuwa mchezaji wa kiwango cha juu nchini England miaka ya tisini , aliuzwa katika klabu cha Inter Milan mnamo mwaka 1995, baada ya bosi wa Mashetani wekundu wakati ule, Sir Alex Ferguson kuamua kwamba Nicky Butt na Roy Kean watakuwa viungo wake wa kwanza.

Rooney mwenye umri wa miaka 27, ameachwa katika kikosi cha Manchester United kilichokwenda Stockholm Sweden katika ziara ya michezo, kutokana na kuwa na maumivu ya bega.