Tuesday 6 August 2013

WAYNE ROONEY KWENDA CHELSEA AMA KUBAKI MANCHESTER?



Rooney atakiwa kuondoka Manchester, kama kweli ana nia ya kwenda Chelsea. “Paul Ince”
 
Na. deo Kaji Makomba

Huko barani ulaya mshambuliaji wa kimataifa Wayne Rooney anatakiwa kuonesha nia yake kama kweli anataka kuiacha klabu ya Manchester United na kujiunga na Chelsea ya England katika msimu mpya wa ligi kuu ya soka nchini humo.

Ushauri huo umetolewa na mchezaji wa zamani wa mashetani wekundu timu ya Manchester united, Paul Ince.

Manchester United tayari walikwishasema ya kuwa mshambuliaji huyo hauzwi huku wakikataa ofa ya pili kutoka kwa Chelsea yenye thamani ya pauni milioni 25.

“Kama Wayne anataka kuondoka, hiyo ni juu yake kuharakisha mchakato huo.” Alisema Ince ambaye ni meneja wa timu ya Blackpool.

“Lakini Wayne hajaweka hadharani kama anataka kuondoka ama kubakia na United
Itakuwa ni vizuri kujua nini Wayne Roy anataka.”


 Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Mashetani wekundu, Manchester United, Paul Ince.
 
Paul Ince ambaye pia hivi sasa ni bosi wa Blackpool ya England licha ya kuwa mchezaji wa kiwango cha juu nchini England miaka ya tisini , aliuzwa katika klabu cha Inter Milan mnamo mwaka 1995, baada ya bosi wa Mashetani wekundu wakati ule, Sir Alex Ferguson kuamua kwamba Nicky Butt na Roy Kean watakuwa viungo wake wa kwanza.

Rooney mwenye umri wa miaka 27, ameachwa katika kikosi cha Manchester United kilichokwenda Stockholm Sweden katika ziara ya michezo, kutokana na kuwa na maumivu ya bega.

No comments:

Post a Comment