Sunday 11 August 2013

NI MAUAJI YA KIKATILI JIJINI MWANZA




Mtu mmoja ashambuliwa hadi kufa na wenzake jijini Mwanza.

·        Ni maeneo ya Nyegezi


·        Yaelezwa kuliibuka mzozo miongoni mwao na ndipo marehemu kushambuliwa na wenzake


·        Chanzo cha mzozo huo hakijajulikana.


              



                  Na. deo kaji makomba


Mtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, amepigwa hadi kufa na watu waliodaiwa kuwa na ubishani naye jijini Mwanza.

Tukio hilo la kusikitisha  limetokea jumamosi iliyopita katika maeneo ya Tamali beach Nyegezi jijini Mwanza, ambapo mtu huyo alipigwa hadi kufa.

Kulingana na watu walioshuhudia tukio hlio wamesema kuwa tukio hilo lilitokea maeneo ya Nyegezi, ambapo vijana wapatao watano walikuwa na ubishani ambao haukufahamika chanzo chake hali iliyozusha tafrani huku yakisikika maneno kutoka kwa vijana wenzake kuwa tutakupiga hadi kufa na ndipo walipomshambulia kwa kumpiga kwa ngumi na mawe hadi kupelekea mauti ya mtu huyo ambaye hakuweza kufahamika jina lake.
Wasamalia wema wakiwa wamewaweka chini ya ulinzi watu waliompiga hadi kufa mwenzao ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja


Miongoni mwa mashuhuda walioshuhudia tikio hilo bwana Jumanne Masenza, amekiambia Kisima hiki cha habari ya kwamba, wasamalia wema waliwakamata watu hao na kuwapeleka katika kituo cha polisi Igogo.
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Bwana Ernest Mangu hakuweza kupatikana ili kuzungumzia kama tayari amekwishapata taarifa kuhusiana na tukio hilo na ni nini hasa chanzo chake.

 Pichi hii ikionesha watu wakishuhudia tukio hilo la kikatili, katika eneo la Mkuyuni, jumamosi iliyopita.(picha na Jumanne Masenza wa TBL)

 Hata hivyo juhudi za kumtafuta kamanda huyo wa polisi mkoani Mwanza, bado zinaendelea ili kuweza kukidhi kiu yako ya habari ndugu msomaji.





No comments:

Post a Comment