Friday 29 November 2013

KOMBE LA DUNIA NDANI YA JIJI LA MWANZA

Matukio katika picha.
Wakati kombe la soka la dunia lilipowasili jijini Mwanza nchini Tanzania, ikiwa ni mpango wa shirikisho soka duniani FIFA kulitembeza katika kuhamasisha mchezo huo unaopendwa na watu wengi duniani.




Kikundi cha Mchelemchele cha jijini Mwanza kikitumbuiza kwa ngoma



Kikundi cha Mchele mchele





Kikundi cha ngoma cha Mchelemchele cha jijini Mwanza kikitumbuiza kwenye uwanja wa CCM Kirumba leo mchana  kombe la Dunia lililpowasili uwanjani hapo.



Kikundi cha Bujorwa nacho kilikuwepo


Kikundi cha Bujorwa kikitumbuiza



Na hapa ulifika wakati wa kucheza na nyoka!


Rais Jakaya Kikwete alipowasili uwanjani CCM Kirumba na hapa alikuwa anasalimiana na viongozi mbalimbali.




Ngoma za utamaduni zikiendelea kutumbuizwa na kikundi cha Mchelemchele


Waziri wa Habari,Vijana, utamaduni na michezo Dr. Fenella Mukangara na kulia ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete


Rais Jakaya Kikwete katikati na viongozi wengine wakielekea kwenye jukwaa





Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Eng.Evarist W. Ndikilo nae alikuwepo.



Dr. Fenella Mukangara

Mwakilishi kutoka kwenye kampuni ya Coca cola


Rais Mpya wa shirikisho la soka nchini bw. Jamal Malinzi nae alikuwepo



Mwakilishi kutoka FIFA nae alipata muda akaongea na wakazi waliojitokeza kwa wingi uwanjani hapo CCm Kirumba kuhusu ujio huo wa Kombe la Dunia Nchini Tanzani ikiwa ni mara ya tatu hapa Nchini.



Waziri wa Habari,Vijana, utamaduni na michezo Dr. Fenella Mukangara.



Viongozi kutoka Mwanza kwenye kiwanda cha Coca Cola



Rais Jakaya Kikwete akiteta na wakazi wa jijini Mwanza leo kuhusu ujio huo wa kombe la Dunia


Rais Jakaya Kikwete (kulia) akiliangalia kombe

Rais Jakaya Kikwete akilifunua kombe la Dunia!!!

Rais Jakaya Kikwete akibeba Kombe juu.


Mwakilishi wa Fifa kushoto akimpa Rais Jakaya Kikwete zawadi jukwaani


Rais Jakaya Kikwete akionesha zawadi aliyopewa hapa!!


Picha za pamoja na Kombe la Dunia zilifata!




Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Eng.Evarist W. Ndikilo akipiga picha na Kombe la Dunia.

Viongozi mbalimbali nao walipata picha hapa na Kombe la Dunia.





Rais Jakaya Kikwete akibea kombe la Dunia juu leo kwa mara ya tatu kwenye uongozi wake lilipowasili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza leo mchana.


Rais Jakaya Kikwete akiwa na Kombe la Dunia Jukwaani kwenye uwanja wa CCM Kiumba jijini Mwanza leo.

Umati wa watu waliokusanyika kwenye uwanja huo wa CCm Kirumba Jijini Mwanza kushuhudia kombe hilo la Dunia ambao kwa leo ni kwa mara ya tantu kutua hapa Nchini Tanzania mara yakwanza ni mwaka 2006, 2009 na leo hii 2013 likishuhudiwa kwa mara ya kwanza jijini Mwanza.