·
Vijana
katika ukanda wa Afrika mashariki watakiwa kutokata tamaa.
·
Ubunifu
na kujituma katika kazi yaelezwa ndio nyenzo pekee ya mafanikio: AY.
Na. Deo Kaji Makomba
Katika kuhakikisha vijana wa ukanda wa Afrika mashariki
wanafanikiwa katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi, wametakiwa kuwa wabunifu na
kutokata tamaa katika shughuli zao
mbalimbali za kila siku za kiujasiliamali, ili waweze kufikia malengo yao.
Ubunifu katika kazi na kutokata tamaa yaelezwa ndio nyenzo pekee
ambayo yaweza kuwavusha vijana hao kwenye eneo la ukanda wa Afrika mashariki katika harakati zao za kila
siku za kupambana na maisha.
Changamoto hiyo imetolewa na mwanamuziki wa Tanzania katika
muziki wa kizazi kipya, Ambwene Yesaya, almaarufu kama AY,wakati akizungumza
katika mahojiano maalum na kisima chetu cha habari kupitia mtandao huu, hivi
karibuni.
Mkurugenzi wa Unity Entertainment, Ambwene Yesaya, AY
AY, katika mahojiano
hayo amewataka vijana katika ukanda huu wa Afrika mashariki kutobweteka na
maisha waliyonayo na badala yake kuongeza bidii , kupambana katika kazi na
kuuchukia umasikini ili kuweza kusonga mbele kimaendeleo zaidi.
Katika falsafa yake ya kujituma na kuwa mbunifu zaidi, AY
ameweza kupata mafanikio makubwa kupitia tasinia ya muziki wa kizazi kipya,
ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika sekta tofautitofauti, hali iliyompatia
manufaa kama yeye binafsi ikiwa ni pamoja
na kutengeneza ajira miongoni mwa vijana wa kitanzania.
Tangu kuanza muziki kwa AY mnamo miaka ya tisini wakati huo
akichomoka na rekodi kadhaa ikiwemo Ni raha tu, Machoni kama watu moyoni hawana
utu,zilizomuweka hewani na kudhihirisha kuwa anacho kipaji , amepata mafanikio
makubwa akiwekeza katika ardhi, anamiliki kipindi cha TV na kumiliki kampuni
ambayo inahusika na masuala mazima ya muziki nchini Tanzania ijulikanayo kwa
jina la UNITY ENTERTAINMENT
Hata hivyo AY, ameongeza kusema kuwa, baadhi ya vijana
wamekuwa hawana nidhamu ya kifedha hali inayosababisha baadhi ya taasisi za
kifedha kukosa imani na hivyo kushindwa kutoa mikopo ili kuwawezesha katika
harakati zao za kupambana na maisha ili kuondokana na umaikini miongoni mwa
vijana.