Monday 12 August 2013

KOMBE LA HISANI HUKO ENGLAND




Manchester United bingwa

·         Yaitandika Wigan Athletics


·         Van Persie azidi safisha nyota kwa Moyes, atupia mbili wavuni.



                Na. deo kaji makomba

Huko nchini England mchezaji Robin van Persie, amemuhakikishia bosi mpya wa mashetani wekundu, timu ya Manchester United, David Moyes kuendelea kuwepo na klabu hiyo, baada ya kuanza msimu huu na kikombe cha ngao ya hisani, kufuatia kipigo ilichokitoa kwa timu ya Wigan athletics kwenye uwanja wa Wembley.

Bosi huyo mpya wa Mashtani wekundu hao wa England, Moyes ametumia muda wake katika msimu huu wa kiangazi kujadili majaliwa ya mshambuliaji wayne Rooney, lakini dimbani katika miaka uliopita Van Perie aliyekuwa aliyekuwa mfungaji bora, kwa mara nyingine ameonesha tofauti.

Ilimchukuwa takribani dakika sita, Van Persie kufungua ukurasa wake katika msimu mpya, akiunganisha kwa kichwa kona fupi  iliyochongwa na Patrie Evra.
 Mhambuliaji wa timu ya Manchester United, akifanya yake jumapili iliyopita katika uwanja waWembley, wakati timu yake ilipoibuka na ushindi katika mchezo wa ngao ya hisani.
 
Wakati Van Persie anaongeza goli la pili kwa Manchester United, ingawa ilikuwa imeshinda inamfanya Moyes kufikiria zaidi kibarua chake kipya vile atakavyoendelea nacho akianza na matokeo mazuri

TUKIO LA KUPIGWARISASI KWA SHEKH MPONDA



Shekh Mponda auguguza jeraha la Risasi chini ya ulinzi wa polisi Dar.


·       Kikosi kazi chaundwa kuchunguza tukio hilo


·       Polisi wakana kuhusika kumpiga Risasi Shekh Mponda



              

                  Na. mwandishi wetu dare es salaam.


Chama cha wananchi CUF, kimeitaka serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuchukua hatua  kali za kisheria ikiwemo kuwatafuta na kuwakamata watu waliohusika na tukio la kumshambulia kwa risasi Shekh Ponda Issa Ponda, wakati akitoka katika sala ya hitimisho ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kauli hiyo ya CUF, imetolewa na mwnyekiti wa chama hicho, profesa Ibrahim Lipumba wakati akizungumza na wandishi wa habari jijini Dare es salaam, kuhusiana na tukio hilo la kupigwa risasi kwa Shekh Mponda.

Bwana Lipumba amesema kuwa serikali kupitia vyombo vyake vya dola inapaswa kulifanyia kazi kwa haraka tukio hilo ili kubaini aliyehusika na hatimaye sheria kuchukua mkondo wake, ili kuondoa uwezekano wa kuwepo machafuko ambayo yanayoweza kuwa katika dini.

Jumuiya ya Taasisi za kidini za Kiislamu nchini Tanzania imeitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini na kuwachukulia hatua watu waliompiga risasi Sheikh Ponda Issa Ponda Jumamosi mjini Morogoro, Mashariki mwa nchi hiyo.

Kulingana na taarifa kutoka jijini Dare es salaam, sheikh Mponda mbaye amekuwa katika mivutano ya mara kwa mara na serikali ya Tanzania alipigwa risasi baada ya kutokea vurugu kwenye mkutano wa mawaidha ya baraza la sikukuu ya Idd el Fitr, huko mjini Morogoro.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Alhajj Mussa Kundecha, amewaambia waandishi wa habari mjini Dare es salaam kuwa endapo serikali haitachukua hatua itakayowaridhisha Waislamu, wataamua kufikiria upya mustakabali wao na serikali ya Tanzania.

Sheikh Ponda amelazwa katika hospitali ya taifa, Muhimbili, mjini Dar es Salaam akiuguza jeraha la risasi huku akiwa chini ya ulinzi wa askari kanzu.

Msemaji wa Jeshi la polisi nchini Tanzania, Advera Senso ameiambia kuwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na jukwaa la haki jinai wameunda kikosi kazi kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa tukio hilo huku akikana kuwa Sheikh Ponda alipigwa risasi na polisi.

Senso amewalaumu wafuasi wa Sheikh Ponda kwa kuwazuia askari kumkamata Sheikh huyo kwa kuwarushia mawe; hatua iliyosababisha askari hao kufyatua risasi hewani ili kuwatawanya na hata hivyo wafuasi hao walifanikiwa kumtorosha kiongozi huyo wa kidini.

Taarifa za jumuiya hiyo ambayo inajulikana zaidi Tanzania kama Shura ya Maimamu zinasema kuwa Sheikh Ponda ambaye polisi wanasema walikuwa wakimtafuta kwa tuhuma za kutoa matamko ya uchochezi, alisafirishwa usiku kutoka mji wa Morogoro hadi Dar es Salaam zaidi ya kilomita 200.

Sheikh Ponda kwa sasa anatumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja alichohukumiwa mapema mwaka huu baada ya kukutwa na makosa kadhaa ikiwemo uchochezi wa kuharibu mali za watu.