SPORTS



LIVER WAFANYA MIPANGO KUMSAJIRI KIPA WA SUNDERLAND
·         Ni Simon Mignolet
                
Na. Deo Kaji Makomba

Barani ulaya uongozi wa majongoo wa London timu ya Liverpool wako katika mpango wa kumsajili mlinda mlango wa timu ya soka ya Sunderland, Simon Mignolet kwa dau la paundi milioni tisa, mchakato mzima ukitarajiwa kufanyika wiki ijayo.

Mlindamlango huyo wa kimataifa wa Ubelgij, anatarajiwa anatarajiwa katika viunga vya Merseside katika siku chache zijazo kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya yake na kukamilisha taratibu za mwisho kwa ajili ya kukipiga na Liverpool.

Mlindamlango huyo mwenye umri wa miaka 24, tayari amekwishacheza michezo 101, tangu alipojiunga akitokea katika klabu ya Sint-Truiden ya Ubelgij juni mwaka 2010 kwa dau la paundi milioni 2. 

 Golikipa huyo ambaye alikuwa akivaa jezi namba 11, aliweza kuchezea timu yake ya Sunderland mechi arobaini katika msimu uliopita huku timu yake ikinusulika katika hatari ya kushuka daraja.

Mlinda mlango aliyepo hivi sasa ambaye ndiye chaguo la kwanza la katika kikosi cha Liverpool Pepe Reina mwenye umri wa miaka 30, imebainika kuwa ana husishwa na kutaka kurejea katiaka mabingwa wa soka Uhispania, timu ya Barcelona, ambako ndiko alikoanzia mishemishe za unyanda




  

      MAJUTO NI MJUKUU!



MABONDIA WA TANZANIA WAHUKUMIWA MIAKA 15 JELA NCHINI MAURTIUS:


·        Ni baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha ‘Unga’
·        Ni wale waliokwenda katika katika mashindano ya ngumi Afrika 2008.

Na. Deo Kaji Makomba kwa msaada wa mashirika ya habari

Hatimaye mabondia wanne wa Tanzania, wamehukumiwa miaka 15 kwenda jela huko nchini Maurtius, baada ya kukiri kujihusiha na usafirishaji madawa haram ya kulevya aina ya heroin.

Mabondia hao wameiambia mahaka nchini humo kuwa walikuwa wakisafirisha madawa hayo aina ya heroin hadi Maurtius kwa sababu walikuwa wanahitaji pesa kwa ajili ya kusaidia familia zao.

Wakati wa kukamatwa kwa mabondia hao walikuwa katika mashindano ya ngumi za ridhaa yaliyokuwa yakifanyika katika nchi ya hiyo, iliyopo kwenye visiwa vya bahari ya hindi mnamo mwaka 2008.

Kesi Ramadhani Fills, Nathanael Elia Charles, Ally Rajabu Msengwa na Petro Charles Mwitanga walionekana kama kuwaahidi mabondia hao vijana, wakati wakitiwa mikononi mwa polisi wa kupambana na madawa ya kulevya nchini Maurtius hapo june 2008 wakati wakiwa Hotelini mjini Quatre Bones takribani kilomita 15 ama maili tisa, kutoka katika mji mkuu wa Maurtius, Port Louis, vyanzo vya habari kutoka nchini humo vimeripoti.

“Sisi ni masikini na tuna majukumu ya kifamilia, watoto na wazazi wetu ni wazee ambao wanatutegemea sisi.” Walijitetea mabondia hao. 

Mabondia hao wa Tanzania walikuwa wakitokea nchini, kwenda kushiriki katika mashindano ya ngumi ya Afrika.

Kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya nchini humo, kiliwatia hatiani mabondia hao, baada ya kupata taarifa za kiintelijensia kuwa wanne hao walikuwa wamebeba madawa hayo,mwandishi wa habari wa BBC, Yasine Mohabuth kutoka Port Louis, ameripoti

Mabondia hao wa Tanzania wametiwa hatiani kwa koa la kilogram 4 za dawa hiyo haram aina ya heroin .

“Tunaomba radhi kwa taifa la Mauritius,” mabondia hao wamesema kabla ya kauli tumefikia mwiho.

“Sisi ni masikini na tuna majukumu ya kifamilia na kazi hii kusafirisha tulikuwa tulipwe Euro 4000, sawa na dola 5,200”

Hukumu hiyo imetolewa na jaji Marie Joseph.



 HABARI ZA MICHEZO MOTOMOTO HUKO MAJUU
           
 Na. Josephat Kaira

 Kiuongo wa timu ya soka ya Barcelona ya Hispania Thiago Alcantara.

Kule nchini Uspania, mlinzi mahiri wa klabu ya soka ya Barcelona ya nchini humo, Gerald Pique, amempa somo mchezaji mwenzake Thiago Alcantara, kuendelea kubakia Barcelona, licha ya kupewa dili ya kujiunga na Mashetani wekundu wa England, timu ya Manchester United kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya soka ya England.

Pique ameongeza kusema kuwa Thiago mzaliwa wa nchini Italia, ambaye amekuwa hapati nafasi ya kucheza kiungo katika kikosi cha kwanza cha Barcelona kutokana na ushindani uliopo kutoka kwa wachezaji wengine ndani ya timu hiyo kama Xavi na Andrea Iniesta, hatakiwi kukata tamaa kwa wakati huu wakati angali chipkizi.

Itakumbukwa ya kwamba kiuongo Thiago mwenye umri(22), ameanza katika kikosi cha kwanza cha Barcelona kwa kucheza mechi 15 katika msimu uliopita wa ligi kuu ya soka ya nchini Uispania.

Thiago Alcantarra ambaye Barcelona iliweka kipengele kwenye mkataba wake kinachoitaka timu yoyote inayotaka kumsajili kulipa paundi milioni 90, anaweza kuuzwa kwa bei ya chini zaidi ya hapo baada ya kucheza mechi zisizozidi 15 msimu uliopita na Thiago mwenyewe anataka kwenda mahali ambako atakuwa na uhakika wa kucheza kwenye kikosi cha kwanza.

Barcelona inamtazama Thiago kama mrithi wa nafasi ya Xavi kwenye kikosi chake lakini wanataka mchezaji huyo avumilie kukaa benchi kwa muda zaidi wakati mkongwe huyo (Xavi) akiwa bado kwenye kiwango chake ambapo pia kocha wa Man United David Moyes amekuwa akimfuatilia Thiago kwa muda mrefu tangu akiwa Everton japo alikuwa akifahamu kuwa Everton haina uwezo wa kumnunua.

 




 LICHA KUFUNGWA 4-2 NA IVORY COST, HARAKATI ZA KWENDA BRAZIL

 ·     Watanzania wasema wana matumaini na Stars ya sasa kufanya vyema siku za usoni.
·         Wataka kutiliwa mkazo kwa soka la vijana na kwamba lolote linawezekana.

         

Na. Deo Kaji Makomba

Licha ya timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa stars, kufungwa mabao 4-2 na timu ya soka ya taifa ya Ivory Cost katika mechi ya harakati ya kuwania kuelekea katika fainali za kombe la dunia  huko nhini Brazil hapo mwakani, wapenzi na mashabiki wa soka nchini Tanzania, wamelezwa kuridhishwa na kiwango cha soka ilichokionesha stars katika mchezo huo hapo jana.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti na kisima cha habari katika mtandao huu wapenzi na mashabiki wa soka wamesema kuwa, hivi sasa wanamatumaini makubwa na kikosi cha stars kutokana na michezo timu hiyo iliyocheza huku ikionesha kiwango kizuri na kwamba Stars inaweza kwenda mbali endapo mipango endelevu juu ya timu hiyo ikiendelea kutiliwa mkazo.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka mkoani Mbeya, mmoja wa mashabiki wa soka, Alex Mkelemi, amesema  kuwa kiukweli Stars hivi sasa inaonesha kuendelea kuimarika siku hadi siku na kuonesha kiwango kizuri licha ya kuwepo makosa madogomadogo kiufundi ambayo hata hivyo ameongeza kuwa mwalimu anaonekana kuyarekebisha kadri siku zinavyokwenda.


Picha ikionesha mchezaji wa stars na Ivory Cost kwenye hekaheka za kuwania tiketi ya kwenda Brazil hapo mwakani, ambapo Stars ililala 4-2, uwanja wa taifa Dar.

Kutokana na hali hiyo, Mkelememi ameongeza kusema kuwa dalili ya Tanzania kuanza kufanya vizuri katika medani ya soka ulimwenguni imeanza kuonekana ila kinachotakiwa ni kutilia mkazo mpango endelevu wa timu hiyo ikiwemo kuwekeza katika soka la vijana ambao ndio watakaokuwa askari wa kesho katika kikosi cha stars.

Naye John Ezekiel mwanafunzi wa chuo cha biashara CBE, Campus ya Mwanza, akizungumza na mtandao huu mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo hapo jana, alisema kuwa kuna mabadiliko makubwa katika kikosi cha Stars hivi sasa, kutokana na  uchezaji wa timu hiyo tofauti na miaka takribani kumi iliyopita.

Jonh alisema kuwa wachezaji wa stars hivi sasa wanajiamini wanaweza kumiliki mpira na kutengeneza nafasi na hatimaye kuzitumia vyema na kupata magoli, ingawa bado kuna hali Fulani ya kukosa uzoefu kitu ambacho wakiendelea kujengewa wanaweza wakafanya makubwa siku za usoni na hatimaye Tanzania kuondokana na kichwa cha mwendawazimu kunako medani ya soka.

Safari ya stars kuwania tiketi ya kuelekea huko nchini Brazil hapo mwakani katika fainali za kombe la dunia, iliishia njiani pale kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, baada ya kuvurugiwa mipango ya safari hiyo na tembo wa Ivory Cost kwa kufungwa mabao 4-2, huku stars ikianza kulisabahi lango la tembo hao dakika ya kwanza tu ya mchezo lililotiwa wavuni na Amri Kihemba na kuamsha hoihoi na ndelemo miongoni mwa mashabiki waliohudhuria mchezo huo jumapili iliyopita.

Picha ikionesha umati wa watazamaji walijitokeza kuangalia mechi kati ya Stars na Ivory Cost uwanja wa taifa Dar.

Hata hivyo Ivory Cost ilisawazisha bao hilo na badae kuongeza la pili, lakini wakiwa hawajakaa sawa Stars ilisawazisha kupitia kwa Thomas Ulimwengu akiunganisha krosi nzuri kutoka kwa Shomari Kapombe.


Mambo yalibadilika na Ivory cost kuonesha uwezo wao kutokana na uzoefu walionao na hatimaye kufanikiwa kupata mabao mawili mengine na kuondoka uwanjani kwa ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Stars katika mchezo huo.

Kwa matokeo hayo Ivory Cost imefanikiwa kuelekea huko nchini Brazil hapo mwakani baada ya kuongoza kundi lake kwa kuwa na pointi 13 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote katika kundi lake huku Tanzania ikiendelea kuwa na pointi 6 huku ikibakiza mchezo mmoja na Gambia, na hivyo kufifisha matumaini ya kuendelea na harakati za kuwania tiketi ya safari ya kuelekea nchini brazil.


No comments:

Post a Comment