Monday 25 November 2013

WATAKAOSHINDWA KULIPIA GHARAMA MPYA ZA UMEME WANUNUE KIBATARI ASEMA NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI TANZANIA

Naibu waziri wa nishati na madini nchini Tanzania anayeshughulikia nishati, Bw. Simba Chawene


Wakati mgao wa umeme ukiendelea nchini Tanzania.
·    Serikali nchini humu yabariki TANESCO kupandisha bei ya umeme.
·    Yadai atakayeshindwa kumudu gharama hiyo anunue kibatari.

Naibu Waziri wa umeme, Mh George Simbachawene, amesema kwamba serikali imekubali TANESCO waongeze gharama za umeme kwa 68% kama walivyokuwa wameomba.

 Alisema hayo wakati akiongea katika kipindi cha Kumepambazuka kupitia Radio One leo asubuhi. 

Amesema kwamba hata kama TANESCO wakiongeza gharama za umeme hadi kufikia Tsh 800 kwa unit bei hiyo ni nafuu kuliko gharama za kununua mafuta ya taa.

Mh Simbachawene ametahadharisha kwamba kama mtu ataona kwamba gharama za umeme ni kubwa, basi akawashe kibatari au akae gizani.

Chanzo cha habari hii ni Kumepambazuka ya Radio One.