Monday 19 August 2013

MANDAMANO YA CHADEMA “YAINUKISHA” MWANZA.



Askari polisi wakiwa kazini kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA
 
Polisi walazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA.

·        Ni baada ya wafuasi wa CHADEMA kukataa kutii amri ya polisi
·        Hali ya hewa yachafuka na shughuli za simama kwa muda jijini Mwanza.
                                    
                              Na. deo kaji makomba.

Polisi mkoani Mwanza wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo, CHADEMA, waliokuwa wamekusanyika katika viwanja vya furahisha jijini Mwanza, kufuatia mandamano ya amani yaliyofanyika jumatatu hii yakianzia katika viwanja vya shule ya msingi Buzuruga  hadi katika viwanja vya furahisha Kirumba.

Mandamano hayo ya wafuasi wa CHADEMA, yaliyoongozwa na mbunge wa Ilemela Bw. Hines Kiwia pamoja na mbunge wa jimbo la Nyamagana Bw. Ezekiel Wenje yalikuwa na lengo la kushinikiza kung’olewa madarakani kwa meya wa manispaa ya Ilmela, Bw. Henry Matata anayedaiwa  kuchaguliwa kinyume cha sheria pamoja na kupinga kufukuzwa kinymela kwa madiwani watatu wa chama hicho.

Madiwani waliofukuzwa na meya wa manispaa ya Ilemela kinyume cha sheria ni Abubakar Kapera diwani wa kata ya Nyamanoro, Marietha Chenyenge(Ilemela) na Dan Kahungu diwani wa kata ya Kirumba jijini Mwanza.
Viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao wakiandamana kutoka Buzuruga kuelekea Viwanja vya Furahisha
 
Mandamano hayo yalianza kwa amani na utulivu majira ya saa tano asubuhi, katika viwanja vya hule ya msingi Buzuruga, yakipita katika barabara ya nyerere, Rufiji, balewa na hatimaye kufika katika viwanja vya furahisha huku yakisimamiwa na walinzi wa usalama, jeshi la polisi mkoani Mwanza.

Baada ya kufika katika viwanja vya furahisha uongozi wa CHADEMA, ukiongozwa na Mbunge wa Ilemela, Bw. Hines uliwataka wafuasi wa chama hicho kutulia katika viwanja hivyo vya furahisha kirumba ili wamfuate mkuu wa mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, aweze kupokea mandamano hayo.

Lakini baada ya uongozi wa CHADEMA kufika katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, walipata fursa ya kuonana na mkuu huyo wa mkoa na kueleza adhima ya mandamano hayo na kwamba kuna taarifa ya kuwepo naarifa kutoka kwa Waziri mkuu na waziri wa serikali za mitaa  TAMISEMI ikiueleza uongozi wa mkuu wa mkoa kuhusiana sakata hilo.
 Picha ikionesha wafuasi wa CHADEMA wakiwa katika viwanja vya furahisha kirumba jijini Mwanza

 Mmoja wa wafuasi wa CHADEMA akionesha msisitizo katika mandamano hayo

 Uongozi huo wa CHADEMA baada ya kufika katika ofisi ya  mkuu wa mkoa Mwanza  ulimtaka kutoa tamko mbele ya wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wakisubilia katika viwanja vya Furahisha.

Akizungumza mbele ya wandishi wa habari na uongozi wa CHADEMA ofisini kwake, Bw. Ndikilo alisema kuwa yeye hajapata taarifa yoyote ya kimandishi iliyoandikwa na waziri mkuu ya kuelekeza kuhusiana na suala hilo la kurejeshwa katika uongozi madiwani hao pamoja na sakata la meya Matata, na kuwataka WANACHADEMA, wasifanyie kazi taarifa ambazo haziko katika mandishi.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, mkuu wa mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo akiongea na viongozi wa CHADEMA ofisini kwake
 Viongozi wa CHADEMA wakiwa wamewasili kwenye viwanja vya furahisha

Aidha Bw. Ndikilo aliwashauri viongozi hao wa CHADEMA, akiwemo mbunge wa ilemela Bw. Hines kwa pamoja na mkuu wa mkoa na mbunge wa Ilemela waende katika ofisi waziri wa wizara husika ili kulifuatilia suala hilo.

Lakini wakati mjadala huo ukiendelea huku nyuma wafuasi wa CHADEMA, waliokuwa katika viwanja vya Furahisha waliamua kwenda kwenye ofisi ya mkoa na ndipo polisi walipowazuia wafuasi hao na kuwataka watawanyike lakini wafuasi wa CHADEMA hawakukubaliana na kauli hiyo huku wakitaka kuelekea katika ofisi ya mkuu wa mkoa na ndipo mambo yalipobadilika kwa kwa polisi kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wafuasi hao.
Tayari kimeanza kimeanza "kunuka"
Polisi wakizima moto uliokuwa umewashwa na wafuasi wa CHADEMA
Barabara ikiwa imewekewa vizuizi wakati wa vurugu hizo jijini Mwanza
Polisi wakiwa kazini
Kama kawaida kazini polisi wakifanya yao
Mama huyu ni miongoni mwa wafuasi wa CHADEMA, aliyejitokeza katika mandamano hayo yaliyokuwa na lengo la kushikiza meya wa Halmashauri ya Ilemela Bw. Matata aondolewe madarakani(Picha na Deo Kaji Makomba)