Saturday 3 August 2013

MASHAKA MAKUBWA YAIBUKA MIONGONI MWA WASANII CHIPUKIZI NCHINI TANZANIA

Msanii wa vichekesho na muziki wa kizazi kipya Rashidi Mwishehe Said wa Mzanga, almaarufu Kingwendu, akizungumza katika mahojiano maalumu na Kisima cha habari hivi karibuni wakati akiwa jijini Mwanza. Hapa akizungumza na muhariri mkuu wa Kisima cha habari, Deo Kaji Makomba.


WASANII WANAOIBUKIA KATIKA FANI YA SANAA YA UIGIZAJI NA MUZIKI NCHINI TANZANIA BAADHI YAO WAKO KATIKA HATARI KUBWA YA MAAMBUKIZI YA UKIMWI.

·        Yaelezwa wengi wao wajitumbukiza katika sanaa kwa lengo la kutafuta  umaarufu na “Mademu”
·        Watakiwa kuwa makini.

                  Na. deo kaji makomba

Wasanii katika nyanja tofauti ya sanaa ikiwemo sanaa ya maigizo na muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, wametakiwa kutumia fani hiyo ya sanaa katika malengo mazuri na si kuingia katika fani hiyo  kwa lengo la kutaka kujipatia umaarufu na mambo yasiyofaa.

Bila kuzingatia misingi na kufanya kazi ya sanaa kwa malengo mazuri wasanii waliojitumbukiza katika fani hiyo kwa malengo ya kutaka kujipatia umaarufu na sifa zisizokuwa na msingi, wako katika hatari kubwa ya kuporomoka na hata kuugua gonjwa hatari la ukimwi.

Kauli hiyo imetolewa na msanii  maarufu  wa vichekesho nchini Tanzania, Rashidi mwinyishehe Saidi wa Mzanga, almaarufu Kingwendu, wakati akizungumza katika mahojiano maalumu na Kisima hiki cha habari jijini Mwanza, hivi karibuni.

 Msanii wa vichekesho na muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Kingwendu, kulia akifuatiwa na mtangazaji wa kituo cha radio cha Metro Fm cha jijini Mwanza, Tony, akifuatiwa na mmoja wa wakurugenzi wa VYUKA SOLUTION, Martin, na aliye na headphone ni mtangazaji nguri wa muziki wa zamani Jacob Usungu, wakati Kingwendu alipotembelea kituo hicho cha radio.

Kingwendu amesema kuwa kumekuwepo na wimbi la vijana wengi hivi sasa nchini Tanzania kujitumbukiza katika fani  ya sanaa ya maigizo muziki na vichekesho, ili kuweza kuona nao wanajikwamua kimaisha kutokana na tasinia hiyo, lakini baadhi yao wamekuwa wakiingia humo kwa ajili ya kujitafutia umaarufu usiokuwa na msingi ikiwemo kujitafutia “mademu” na kufanya umalaya.

Kingwendu ambaye pia ni  msanii wa muziki wa kizazi kipya, ameongeza kusema kuwa sanaa hahiitaji kuifanyia mambo mabaya kwani ni kitu ambacho kimeweza kutengeza ajira kwa vijana wengi nchini Tanzania na kuondoa dhana potofu iliyokuwa imetanda kunako miaka ya nyuma kuwa fani ya muziki na maigizo pamoja na vichekesho ilikuwa  ni uhuni.

 Kingwendu akiwa katika pozi, wakati alipotembelea Metro Fm jijini Mwanza hivi karibuni(Picha zote na maktaba ya Kisima cha habari)

Aidha Kingwendu ambaye pia aliwahi kutikisa na rekodi kadhawakadha za muziki ikiwemo wimbo wake wa Huyu demu ana mapepe.

Waweza sikiliza mahojiano maalum kati ya Kingwendu na na Deo Kaji Makomba wa Kisima cha habari yaliyofanyika hivi karibuni.>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>