Saturday 1 February 2014

HARAKATI ZA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA, MAN CITY KUMKOSA AGUERO>>>>>>>>>>>>>



Sergio   Aguero
Manchester City kumkosa Aguero.
·    Ni katika mechi ya ligi ya mabingwa barani ulaya.
·    Majeraha yamsababisha kukaa nje. Nako nchini Uhispania kocha wa zamani wa soka wa timu ya taifa ya nchi hiyo afariki dunia.

                                              Na. Josephat Kaira.

Kama  kawaida kisima cha burudani kinaendelea kukutaarifu  kuhusiana na  dondoo mbalimbali  za soka kimataifa   ambapo   tukianzia  Uingereza   kunataarifa kutoka  ndani  ya   Klub ya  Mancheter city   ya kuwa   itamkosa  mchezaji wake  Sergio   Aguero   katika  mechi ijayo ya kombe  la mabingwa wa soka barani   ulaya kufuatia  kuwa  majeruhi.

Tayari meneja wa mancheter city  Manuel  Mellegrin    amethibitisha ya  kuwa  Aguero atakaa  nje ya dimba kwa kipindi cha mwezi   mmoja baada  ya  kupata maumivu ya nyonga katika mechi iliyopita dhidi ya tottenham  jumatano iliyopita.

Kutokana na  kuwa majeruhi Aguero  ataikosa mechi  dhidi   ya  Baselona inayotarajiwa kuchezwa februari   18.

Nako nchini Hispania  jumamosi hii   kumeripotiwa  taariafa ya  huzuni  ikimhusu   aliyewahi kuwa kocha wa  timu ya taifa ya nchi hiyo   Luis  Aragones  kufariki dunia mapema asubuhi ya  leo  katika clinic ya  mjini Madrid.
  Luis  Aragones

Taarifa ya kufariki kwa  Aragones   imetolewa  na   dactari   aliyekuwa akimtibu    Pedro   Guiren   ,Aragones ambaye  alikuwa akifahamika kama  Wise man  aliiongoza   Uispania   katika michuaano ya soka  ya ulaya ya mwaka  2008

Aragones   amefariki akiwa na miaka    75   na atataendelea kubaki katika    kumbukumbu ya wapenda  soka  duniani.

Naye bosi wa  timu ya soka ya taifa ya uholanzi Ruiz Van gaal  amethibitiha kuwa amechoka na anafikiria kuustafu kufundisha mchezo wa soka,  mara baada ya kumalizika kwa  michuano ijayo ya kombe la dunia  katikati ya mwaka huu huko  nchini brazil.
 Ruiz Van gaal

Van gaal   ameongeza kuwa miaka miwili aliyokaa kama kocha wa timu ya uholanzi amekuwa kama mgonjwa na amechoka na kibarua hicho  na amefikiria  utakuwa muda muafaka kwake kupumzika mara baada ya kumalizika kwa michuano hiyo ya soka mikubwa duniani.

Nchini  ufaransa kiungo wa  Klub ya  Paris saint german  Blaise  Matuidi  amebainisha   kuwa   yuko kwenye mipango ya kusaini mkataba mpya kuendelea kubaki kwenye Klub hiyo ya nchini ufaransa.
 Blaise  Matuidi

Kiungo Blaise mwenye umri wa miaka 26 amesema ya kuwa anafurahia kuendelea kubakia  Psg  na hakuna ukweli wowote  wa kuwa yuko kwenye mipango ya kutimkia Aserna l ya Uingereza kama ilivyokuwa ikiripotiwa awali.

Naye bosi  Klub ya Fayenoord   Ronard Koeman ameweka  hadharani kuwa ataachana na kibarua cha kuinoa timu hiyo ya uholanzi mwishoni mwa  msimu huu,itakumbukwa ya kuwa koeman amekuwa clubuni hapo kwa muda wa miaka mitatu tangu ajiunge nayo mwaka  2011 akichukua nafasi ya Mario been.
Ronard Koeman
 
Kocha huyo wa fayenoord amesisitiza kuwa anaelewana na kila mmoja kwenye  club hiyo ila ni maamuzi yake binafsi  aliyofikia ya kutosaini mkataba mpya na timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya uholanzi.

SOKA KIMATAIFA


                                                    Na. Josephat Kaira.



NA  HUU NI  MKUSANYIKO  WA HABARI  MBALIMBALI   ZA  MICHEZO   ZA  KIMATAIFA   TUNAANZIA NA TAARIFA  KUTOKA  NDANI  YA CLUB YA   CHELSEA   YA  ENGLAND  IMEKAMILISHA  USAJILI  WA  MLINZI  WA  KATI  KURT    ZOUMA   KUTOKA CLUB   YA   ST  ETIENE YA  NCHINI UFARANSA.

MLINZI   ZOUMA    AMESAINI  MKATABA  WA  MIAKA  MITANO   NA   NUSU   KUICHEZEA  CHELSEA  LAKINI  ATABAKIA  KATIKA   CLUB   HIYO YA   UFARANSA  HADI  MWISHO WA  MSIMU    HUU.
 

Kurt Zouma

ITAKUMBUKWA  YA KUWA  ZOUMA   ALIJIUNGA   ST  ETIENE   MWAKA   2009  AMEICHEZEA  MECHI  52  NA KUIFUNGIA MABAO MANNE.

CHELSEA    IMELAZIMIKA  KUTOA  KIASI   CHA    PAUNI  MILIONI  12    KUFANIKISHA    USAJILI    WA  MLINZI   ZOUMA.

-NAYO   CLUB   YA  SOKA  YA WESTHAM  IMEMAJILI    KWA  MKOPO    MLINZI  PABLO  ARMERO KUTOKA  CLUB  YA   NAPOLI YA   NCHINI   ITALIA,MLINZI HUYO  ANAYEMUDU  KUCHEZA  NAFASI  YA  MLINZI WA  KUSHOTO  RAIA   WA  COLOMBIA  ATALAZIMIKA  KUSUBIRI  HADI  MWISHO  WA MSIMU    HUU KUJIUNGA  NA WAGONGA  NYUNDO HAO WA  LONDON.

 Pablo Armero

-NAYO   LIGI   KUU YA   SOKA   YA   ENGLAND ITANDELEA TENA   LEO JUMAMOSI   KWA   MECHI   SABA  NEWCASTLE     ITAIKARIBISHA    SANDALEND   WAKATI  WESTHAM UNITED    WATAKUWA  DIMBANI KUWAKABILI   SWANZ.

KATIKA    MECHI NYINGINE  ZA  LIGI  KUU  YA  ENGLAND   JUMAMOSI  HII    CARDIF  CITY   ITAIKABILI     NORWICH     WAKATI  EVATON ITAIKABILI  ASTON   VILLA    VILIE   VILE    FULHAM     SOUTHAMPTON.

-NAYE   KIUNGO WA   KIMATAIFA  WA COSTARICA    BRAYN  OVIEDO  AMEFANYIWA   OPARESHENI    YA   MGUU   ILIYOELEZEWA KUWA  YA  MAFANIKO   WAKATI   TAIFA  LAKE  LIKIWA  KATIKA  MAANDALIZI YA  KUSHIRIKI  KOMBE LA DUNIA   MAPEMA MWAKA HUU  NCHINI   BRAZIL.
 Bryan Oviedo

KIUNGO   OVIEDO   ALIUMIA    KATIKA   MECHI   YA KOMBE   LA FA   BAINA   YA  TIMU YAKE  YA EVATON  DHIDI    YA    TIMU  YA  STEVAGE.

-NAKO  NCHINI   HISPANIA   CLUB   YA  BASELONA  IKO  KWENYE  MIPANGO  YA   KUMSHAWISHI  MLINDA  MLANGO WAKE   VICTOR   VALDES  KUSAINI  MKATABA  MPYA   WA   KUENDELEA  KUKIPIGA   NA CLUB  HIYO.
  Victor Valdes

ITAKUMBUKWA YA KUWA   VALDES  ALIKWISHA   TANGAZA KUWA  ATAONDOKA  BAELONA  MARA  BAAADA YA MKATABA WAKE    WA   SASA  KUMALIZIKA.

NAYO  TIMU  YA RACING  SANTANDA IMEFUNGIWA   KWA KIPINDI  CHA MWAKA  MMOJA KUTOSHIRIKI MICHUANO  YA KOMBE  LA   COPA DE REY KUFUATIA  KUUGOMEA  MECHI  YAO   DHIDI YA  REAL  SOCIADAD,RACING ILIGOMEA  MECHI  HIYO ALHAMIS ILIYOPITA  KUTOKANA  NA WACHEZAJI WAKE   KUTOLIPWA   MISHAHARA YAO  PAMOJA NA KUFUNGIWA  HUKO PIA CLUB HIYO IMETOZWA  KIASI CHA  YURO 3006 KUTOKANA NA KOSA HILO.
 Racing Santander