Saturday 1 February 2014

HARAKATI ZA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA, MAN CITY KUMKOSA AGUERO>>>>>>>>>>>>>



Sergio   Aguero
Manchester City kumkosa Aguero.
·    Ni katika mechi ya ligi ya mabingwa barani ulaya.
·    Majeraha yamsababisha kukaa nje. Nako nchini Uhispania kocha wa zamani wa soka wa timu ya taifa ya nchi hiyo afariki dunia.

                                              Na. Josephat Kaira.

Kama  kawaida kisima cha burudani kinaendelea kukutaarifu  kuhusiana na  dondoo mbalimbali  za soka kimataifa   ambapo   tukianzia  Uingereza   kunataarifa kutoka  ndani  ya   Klub ya  Mancheter city   ya kuwa   itamkosa  mchezaji wake  Sergio   Aguero   katika  mechi ijayo ya kombe  la mabingwa wa soka barani   ulaya kufuatia  kuwa  majeruhi.

Tayari meneja wa mancheter city  Manuel  Mellegrin    amethibitisha ya  kuwa  Aguero atakaa  nje ya dimba kwa kipindi cha mwezi   mmoja baada  ya  kupata maumivu ya nyonga katika mechi iliyopita dhidi ya tottenham  jumatano iliyopita.

Kutokana na  kuwa majeruhi Aguero  ataikosa mechi  dhidi   ya  Baselona inayotarajiwa kuchezwa februari   18.

Nako nchini Hispania  jumamosi hii   kumeripotiwa  taariafa ya  huzuni  ikimhusu   aliyewahi kuwa kocha wa  timu ya taifa ya nchi hiyo   Luis  Aragones  kufariki dunia mapema asubuhi ya  leo  katika clinic ya  mjini Madrid.
  Luis  Aragones

Taarifa ya kufariki kwa  Aragones   imetolewa  na   dactari   aliyekuwa akimtibu    Pedro   Guiren   ,Aragones ambaye  alikuwa akifahamika kama  Wise man  aliiongoza   Uispania   katika michuaano ya soka  ya ulaya ya mwaka  2008

Aragones   amefariki akiwa na miaka    75   na atataendelea kubaki katika    kumbukumbu ya wapenda  soka  duniani.

Naye bosi wa  timu ya soka ya taifa ya uholanzi Ruiz Van gaal  amethibitiha kuwa amechoka na anafikiria kuustafu kufundisha mchezo wa soka,  mara baada ya kumalizika kwa  michuano ijayo ya kombe la dunia  katikati ya mwaka huu huko  nchini brazil.
 Ruiz Van gaal

Van gaal   ameongeza kuwa miaka miwili aliyokaa kama kocha wa timu ya uholanzi amekuwa kama mgonjwa na amechoka na kibarua hicho  na amefikiria  utakuwa muda muafaka kwake kupumzika mara baada ya kumalizika kwa michuano hiyo ya soka mikubwa duniani.

Nchini  ufaransa kiungo wa  Klub ya  Paris saint german  Blaise  Matuidi  amebainisha   kuwa   yuko kwenye mipango ya kusaini mkataba mpya kuendelea kubaki kwenye Klub hiyo ya nchini ufaransa.
 Blaise  Matuidi

Kiungo Blaise mwenye umri wa miaka 26 amesema ya kuwa anafurahia kuendelea kubakia  Psg  na hakuna ukweli wowote  wa kuwa yuko kwenye mipango ya kutimkia Aserna l ya Uingereza kama ilivyokuwa ikiripotiwa awali.

Naye bosi  Klub ya Fayenoord   Ronard Koeman ameweka  hadharani kuwa ataachana na kibarua cha kuinoa timu hiyo ya uholanzi mwishoni mwa  msimu huu,itakumbukwa ya kuwa koeman amekuwa clubuni hapo kwa muda wa miaka mitatu tangu ajiunge nayo mwaka  2011 akichukua nafasi ya Mario been.
Ronard Koeman
 
Kocha huyo wa fayenoord amesisitiza kuwa anaelewana na kila mmoja kwenye  club hiyo ila ni maamuzi yake binafsi  aliyofikia ya kutosaini mkataba mpya na timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya uholanzi.

No comments:

Post a Comment