Wednesday 4 September 2013

PILIKAPILIKA ZAENDELEA UWANJA MKONGWE NYAMAGANA

 Picha ikionesha watu mbalimbali wakishuhudia maonesho ya biashara kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Ni katika maonesho ya biashara ya kimataifa ya nchi za ukanda wa Afrika mashariki

  • Watu mbalimbali wamiminika kushuhudia maonesho hayo

  • Yafunguliwa rasmi na mkuu wa mkoa Mwanza.

                           Na, deo kaji makomba

Pilikapilika ndani ya uwanja mkongwe jijini mwanza zinazidi kupamba moto huku watu mbalimbalimbali wakijivinjari katika uwanja huo kushuhudia maonesho makubwa ya biashara ya kimataifa yaliyoanza jumamosi iliyopita.

Maonesho hayo ya biashara ya kimataifa ni ya nane kufanyika jijini humu yakiandaliwa na chama chama wafanyabiashara mkoani Mwanza, TCCIA, na huku yakishirikisha nchi kutoka ukanda wa Afrika mashariki ikiwemo kenya, Uganda na mwenyeji Tanzania.

Nazo nchi kutoka Singapore, Misri zinashiriki kwenye maonesho hayo kama nchi waalikwa,
Tayari maonesho hayo yamefunguliwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, huku akiwasisitiza wafanyabiashara kutumia fursa zilizopo katika maonesho hayo ili kufika mbali katika shughuli nzima za kibiashara.

Hapa chini ni matukio katika picha kwenye maonesho hayo ya biashara ya kimataifa yanayoendelea kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana jijini Mwanza.(Picha zote na deo kaji Makomba)