Friday 21 June 2013

ARDO KING FT PASSION - ALL I HAVE (OFFICIAL MUSIC VIDEO)


ARDO KING SIMPLE, AACHILIA HEWANI VIDEO YA “ALL I HAVE” HUKO MAREKANI.


·       Mipango yafanywa video hiyo kuonekana TV za Bongo
·       Mwana hip hop wa kweli nayo yaendelea kufanya vyema katika vituo mbalimbali vya Radio.

Na. Deo Kaji Makomba

Baada ya mtanzania anayefanya muziki wa Hip hop nchini Marekani, Eliatosha Adonia , almaarufu Ardo King simple, kuachilia hewani rekodi ya Mwana hip hop wa kweli katika vituo mbalimbali vya redio nchini Tanzania, huku rekodi hiyo ikiendelea kufanya vyema katika vituo hivyo, mwanamuziki huyo hivi sasa ameachilia hewani Video ya wimbo wake wa All I HAVE.

Katika rekodi hiyo aliyoiimba kwa lugha ya kiingeeleza na kurekodiwa nchini Marekani na kumshirikisaha mwanamuziki wa miondoko ya R&B wa nchini humo, Passion, Video yake imefanywa  na kampuni ya DIMINSIONS ENTERTAINMENT .
Tayari video hiyo inaonekana hivi sasa katika mtandao wa You tube, huku mashabiki mbalimbali wa muziki wakiendelea kutoa maoni na pongezi zao kwa ardo King simple, kutokana na kazi nzuri aliyoifanya katika video hiyo.

Video ya ALL I HAVE, imeachiliwa hewani hii leo katika mtandao wa You tube, ikiwa ni moja ya mkakati wa kumtambulisha mwanamuziki huyo katika tasinia ya muziki kimataifa zaidi, kwa mujibu wa management ya LEGENDARY MUSIC.

Na wakati video hiyo ya ALL I HAVE ikiachiliwa hewani hii leo katika mtandao wa You tube , mipango inafanywa ili kuweza kuisambaza katika vituo mbalimbali vya TV vya hapa nchini ili kuweza kutoa fursa kwa watu wengi kukiangalia kitu katika chupa.

Angalia hapa video ya ALL I HAVE yake Ardo King Simple.....


MABONDIA WA TANZANIA WAHUKUMIWA MIAKA 15 JELA NCHINI MAURTIUS


·        Ni baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha ‘Unga’ aina ya heroin
·        Ni wale waliokwenda katika mashindano ya ngumi Afrika 2008.

Na. Deo Kaji Makomba kwa msaada wa mashirika ya habari

Hatimaye mabondia wanne wa Tanzania, wamehukumiwa miaka 15 kwenda jela huko nchini Maurtius, baada ya kukiri kujihusiha na usafirishaji madawa haram ya kulevya aina ya heroin.

Mabondia hao wameiambia mahaka nchini humo kuwa walikuwa wakisafirisha madawa hayo aina ya heroin hadi Maurtius kwa sababu walikuwa wanahitaji pesa kwa ajili ya kusaidia familia zao. Soma habari hii kwa undani zaidi>>>>Ukurusa wa sports