NEWS


KAGAME NA KIKWETE WAMALIZA TOFAUTI ZAO

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete

Rwanda na Tanzania sasa safi, Kikwete


                                           Na. mwandishi wetu.

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ametangaza kuwa mgogoro baina ya Tanzania na Rwanda umemalizika.

Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi,  Rais Kikwete amesema hatua hiyo inafuatia mazunguzo baina ya viongozi hao wawili yaliyofanyika hivi karibuni nchini Uganda .

Japo hajataja ni kwa namna gani mgogoro huo uliokuwa umefukuta baina ya Tanzania na Rwanda utakuwa umepatiwa ufumbuzi, Rais Kikwete katika hotuba yake amesema kuwa, hatua ya mazungumzo baina yake na Rais wa Rwanda Paul Kagame ndio chanzo cha mafanikio hayo yote.

Tanzania na Rwanda zilingia katika mgogoro wa kidiplomasia hadi kufikia hatua ya kutunishiana misuli kisiri baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzishauri nchi za Rwanda na Uganda kuzungumza na waasi wa nchi zao waliopo nchini Jamuhuiri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Jambo hilo lililopingwa vikali na Rwanda kwa madai kwamba Rais Kikwete aliingilia mambo ya ndani ya Rwanda kwa kuwashauri kufanya mazungumzo na watu walioua raia wa nchi hiyo.

Mgogoro huu ulipamba moto na hata kukolezwa zaidi na vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.
Rais Kikwete ametoa wito kwa vyombo vya habari, wanasiasa pamoja na mitandao ya kijamii kusaidia kwa upande mwingine kuziba ufa wa uhusiano uliojitokeza kati ya nchi hizo mbili.

Aidha katika hotuba rais Kikwete alitumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi wa opereshi ya kuwaondoa wahamiaji haramu nchini humo iliyofanyika hivi karibuni ambapo amesema kuwa operesheni hiyo iliendeshwa bila kukiuka haki za binadamu.
Kuhusu wahamiaji waliokaa nchini Tanzania muda mrefu Rais Kikwete amesema watu hao sasa watepewa uraia rasmi wa Tanzania ili wafuate uratibu.


HALI YACHAFUKA HUKO MOMBASA NCHINI KENYA.


Salim Adbi pekee ndiye aliyenusurika kifo


Ghasia zaibuka huko pwani ya Kenya.

·         Ni baada ya mauaji ya mauaji ya Shekh Logo huko Mombasa.

·         Vijana wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa dini ya kiislam wateketeza kanisa

                            
                                      Na. deo kaji makomba na,mashirika ya habari.

Taarifa kutoka mjini Mombasa pwani ya Kenya zinasema kuwa vijana wameteketeza kanisa katika ghasia ambazo zimezuka kufutia kuuwa kwa muhuburi wa dini ya kiisilamu.

 Inaarifiwa mtu mmoja ameuawa kutokana na  ghasia hizo.

Sheikh Ibrahim Omar aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa na washirika wake wa watatu
Kulingana na taarifa za kipolisi kutoka mjini Mombasa zinaeleza kuwa muhubiri huyo alikuwa akihubiri katika msikiti uliohusishwa na wanamgambo wa kiisilamu wa Al Shabaab. 

Haijulikani aliyetekeleza mauaji hayo ya usiku wa kuamkia ijumaa hii huku kukiendelea kuwa na hali ya wasiwasi miongini mwa waisilamu na maafisa wa usalama mjini humo.

Sheikh Ibrahim Rogo alikuwa muhubiri katika msikiti alipokuwa akihubiri marehemu Sheikh Aboud Rogo ambaye pia aliuawa kwa kupigwa risasi. Aliuawa na watu wengine watatu walipokuwa wanarejea nyumbani Alhamisi usiku baada ya kuhubiri.
 
Sheikh Rogo alishutumiwa kutoa mafunzo yenye itikadi kali yaliyowashawishi vijana kujiunga na makundi ya kigaidi kama Al Shabaab.

Marehemu Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al Shabaab
Mauaji haya ni sawa na ya marehemu Aboud Rogo Mohammed mwaka jana na ambayo yalisababisha ghasia mjini humo. 


                                                    Marehemu Aboud Rogo

Yanakuja wiki mbili tu baada ya shambulizi la kigaidi lililofanywa dhidi ya jumba la maduka la Westgate ambapo watu 67 waliuawa

Kundi la kigaidi la al-Shabab lilikiri kufanya mashambulizi hayo ya kigaidi.

Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Shabab na baadhi ya waisilamu walioshutumu polisi waliomuua walisema kuwa yalikuwa madai tu wala.

Ibrahim Rogo alionekana kama mrithi wa marehemu Aboud Rogo, alipohutubu katika msikiti huo.

 


BADO NI HATARI HUKO NCHINI MISRI




                                Polisi akiwa amewakamata miongoni mwa wafuasi wa Morsi



Hali ya hewa huko nchini Misri bado si shwari.

·        Wafuasi wa Morsi kwa mara nyingine wapambana na polisi


·        Usalama waimarishwa Katika medani ya Tahrir
               
                              Na. deo kaji makomba na mashirika ya habari.

Vikosi vya usalama nchini Misri vimeimarisha ulinzi katika sehemu kadhaa mjini Cairo baada ya vurugu kuzuka kutokana na makabiliano kati ya wafuasi wa Mohammed Morsi na vikosi vya usalama katika mji huo na ule wa Alexandria.

Kwa mujibu wa ripot kutoka katika mashirika mbalimbali ya habari ya kimataifa zinaeleza ya  kuwa milipuko na milio mikubwa ya risasi imesikika katika sehemu za katikati mwa mji mkuu, Cairo.

Kulingana na taarifa hizo, Sehemu ambazo zimezingirwa na polisi ni  zile ambazo wafuasi wa rais aliepindiliwa Mohammed Morsi waliwahi kupiga kambi baada ya Morsi kuondolewa kwa nguvu mamlakani na vikosi vya usalama mwezi Agosti katika operesheni iliyosababisha mamia kadhaa kupoteza maisha.

Pia usalama umeimarishwa karibu na medani ya Tahrir ambako waandamanaji waliokuwa wanapinga Morsi walikusanyika katika maandamano ya kumtaka ajiuzulu kabla ya majeshi kumtoa madarani miezi mitatu iliopita.

Vyombo vya habari vimeripoti kutokea ghasia zaidi katika mkoa wa Kaskazini wa Sharqiya, Mashariki mwa Gaza, pamoja na Kaskazini mwa mji wa bandarini wa Alexandria.

Mamia ya watu wameuwa tangu jeshi kumuondoa mamlakani Morsi mwezi Julai.

Maelfu ya wanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood pia wamezuiliwa katika miezi miwili iliopita.
Baadhi ya maafisa wakuu wa chama hicho akiwemo bwana Morsi na generali Mohammed Badie, wanazuiliwa kwa madai ya kuchochea ghasia na mauaji.

Vuguvugu hilo limelalamika na kusema kuwa maafisa wanazifanya juhudi zao dhidi yao, kuonekana kama vita dhidi ya ugaidi.



20 wauawa kwenye makabiliano Nigeria

Na. Mashirika ya habari


Takriban watu 20 wameuawa nchini Nigeria baada ya makabiliano makali kati ya makundi ya vijana waliojihami na wapiganaji wa kiisilamu.

Hii ni kwa mujibu wa jeshi na vijana wanaotoa ulinzi kwa wanavijiji.

Kulingana na vijana hao wanaotoa ulinzi kwa niaba ya serikali, wapiganaji walivamia kijiji cha Dawashe kaskazini mwa nchi siku ya Jumamosi , kukabiliana na wapiganaji hao wa kiisilamu ambao nao walilipiza kisisasi kwa kutumia silaha nzito huku wakiwaua raia.

Kikundi hicho cha ulinzi kiliibuka mwezi Mei na kuanza harakati zake wakati huo.
Kimeahidi kusaidia serikali kupambana na wapiganaji wa Boko Haram.

Zaidi ya watu 2,000 wameuawa tangu mgogoro huu kuanza mwaka 2009.
Kundi la Boko Haram linasema kuwa linapigana dhidi ya serikali kutaka kuwa na utawala wa kiisilamu kote Nigeria.
 
 Vijana hawa wanaungwa mkono na jeshi na hata wamepewa mafunzo kukabiliana na Boko Haram


Jeshi linatizama wapiganaji hao kama washirika wake na hivyo limewapa mafunzo kulisaidia katika harakati dhidi ya wapiganaji hao wa kiisialamu.

Kiongozi wa vijana hao Aliko Musa alisema kuwa watu 25 waliuawa mjini Dawashe katika jimbo la Borno ambalo ndilo kitovu cha harakati za Boko Haram.

Naye msemaji wa jeshi Haruna Mohammed Sani alithibitisha kuwa watu 20 waliuawa.


No comments:

Post a Comment