Saturday 17 August 2013

MASHINDANO YA ALLIANCE SCHOOL EAST AFRIKA TOURNAMENT.

 Mkurugenzi wa Alliance academy school ya jijini Mwanza, James Bwire, wakati akizungumza na Kisima hiki cha habari.(Picha na Deo Kaji Makomba)


Mashindano ya soka kwa vijana wa Afrika Mashaririki



·       Kuanza kurindima jumapili hii uwanja wa Nyamagana


·       Timu kutoka ukanda wa Afrika mashariki na kati kushiriki mashindano hayo.



                                  

                                      Na. deo kaji makomba.

Mashindano ya soka maarufu kama Alliance school Mwanza east Afrika tournament, yanatarajia kuanza jumapili hii agost 18 mwaka huu kwenye uwanja mkongwe wa Nyamaganaga jijini Mwanza.

Mashindano hayo ya soka yatakayoshirikisha timu za shule za michezo kutoka katika ukanda wa Afrika mashariki na kati yamendaliwa na shule ya Alliance academy iliyopo kata ya Mahina jijini Mwanza.

Kulingana na uongozi mkuu wa wa Alliance academy, shule kutoka Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo pamoja na wenyeji Tanzania zitashiriki katika mashindano hayo yenye lengo la kuwapatia ushindani wachezaji kutoka katika shule ya alliance, lakini pia kujenga mahusiano mazuri miongoni mwa nchi washiriki katika mashindano hayo.

Akizungumza na Kisima chetu cha habari ofisini kwake jijini Mwanza, mkurugenzi wa shule ya Alliance academy, James Bwire, amesema kuwa, jumla ya timu 27 kutoka katika nchi za ukanda huo wa Afrika mashariki na kati zitashiriki katika mashindano hayo.
 Timu ya Alliance academy ikiwa katika mazoezi kujiandaa na mashindano hayo ya Afrika mashariki na kati.

Aidha Bw. Bwire ameongeza kusema kuwa mandalizi yote kuelekea mashindano hayo yamekwishakamilika na kwamba jumapili hii mashindano hayo yataanza kurindima kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana, jijini Mwanza.

Katika mahojiano yake na Kisima cha habari, Bwire ameongeza kusema kuwa milango iko wazi kwa wale wote wenye mapenzi mema kuweza kufadhili mashindano hayo yenye lengo la kuendeleza vipaji vya soka la vijana wa Tanzania ili kuwaweza siku za usoni kuweza kujiali kupitia michezo ikiwemo soka.

Mashindano hayo yanatarajia kufikia tamati hapo Agost 20 mwaka huu.