Friday 30 August 2013

PILIKAPILIKA NDANI YA JIJI LA MWANZA ZAANZA.



Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mwanza, Bw. Elibariki Mmali, akizungumza na wandishi wa habari jijini Mwanza

Ni kutokana na kuanza kwa maonesho makubwa ya biashara ya kimataifa.

·        Makampuni kutoka Kenya, Uganda, Tanzania, China, Misri na Singapore kuonesha bidhaa zao.


·        Mkuu wa mkoa wa Mwanza kuyafungua rasmi septemba 2



 

                                            Na. deo kaji makomba
Maonmesho ya kimataifa ya biashara ya nchi za ukanda wa Afrika mashariki yanaanza ijumaa hii kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana Jijini Mwanza.

Makampuni kutoka nchi za Kenya , Unganda na mwenyeji Tanzania yatashiriki katika maonesho hayo huku nchi za misri, Singapore pamoja na China zikiwa nchi waalikwa kuonesha bidhaa mbalimbali katika maonesho hayo.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na chama cha wafanyabiashara mkoani Mwanza, TCCIA, kupitia mwenyekiti wake Bw. Elibariki Mmali, maonesho hayo ijumaa hii na yakitarajiwa kufunguliwa rasmi jumatatu hii septemba 2 mwaka huu na mkuu wa mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo.

Zaidi ya makampuni 350 kutoka katika nchi za ukanda wa Afrika mashariki pamoja na nchi tatu waalikwa yanatarajia kushiriki maonesho haya ambayo hivi sasa yamefikia mwaka wake wa nane tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2005, yakiwa na lengo la kutoa fursa kwa wajasilia mali wadogowadogo katika nchi hizo kuonesha kazi zao wanazozalisha ikiwa ni pamoja na kutanua wigo biashara zao kupitia maonesho hayo.

Akizungumza mbele ya wandishi wa habari jijini Mwanza katika kuelekea kwenye maonesho hayo, mwenyekiti huyo wa TCCIA, mkoani Mwanza, Bw. Mmali, amesema kuwa makampuni ya nje yaliyokuja na bidhaa kwa ajili ya maonesho tu, hayataruhusiwa kuuza bidhaa hizo kwa kuwa zitakuwa zimeletwa kwa ajili ya maonesho.