Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mwanza, Bw. Elibariki Mmali, akizungumza na wandishi wa habari jijini Mwanza
Ni kutokana na kuanza kwa maonesho makubwa ya biashara ya kimataifa.
· Makampuni kutoka Kenya, Uganda, Tanzania, China, Misri na Singapore kuonesha bidhaa zao.
· Mkuu wa mkoa wa Mwanza kuyafungua rasmi septemba 2
Na.
deo kaji makomba
Maonmesho ya kimataifa ya biashara ya nchi za ukanda wa
Afrika mashariki yanaanza ijumaa hii kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana Jijini
Mwanza.
Makampuni kutoka nchi za Kenya , Unganda na mwenyeji
Tanzania yatashiriki katika maonesho hayo huku nchi za misri, Singapore pamoja
na China zikiwa nchi waalikwa kuonesha bidhaa mbalimbali katika maonesho hayo.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na chama cha
wafanyabiashara mkoani Mwanza, TCCIA, kupitia mwenyekiti wake Bw. Elibariki
Mmali, maonesho hayo ijumaa hii na yakitarajiwa kufunguliwa rasmi jumatatu hii
septemba 2 mwaka huu na mkuu wa mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo.
Zaidi ya makampuni 350 kutoka katika nchi za ukanda wa
Afrika mashariki pamoja na nchi tatu waalikwa yanatarajia kushiriki maonesho
haya ambayo hivi sasa yamefikia mwaka wake wa nane tangu kuanzishwa kwake mnamo
mwaka 2005, yakiwa na lengo la kutoa fursa kwa wajasilia mali wadogowadogo
katika nchi hizo kuonesha kazi zao wanazozalisha ikiwa ni pamoja na kutanua
wigo biashara zao kupitia maonesho hayo.
Akizungumza mbele ya wandishi wa habari jijini Mwanza katika
kuelekea kwenye maonesho hayo, mwenyekiti huyo wa TCCIA, mkoani Mwanza, Bw.
Mmali, amesema kuwa makampuni ya nje yaliyokuja na bidhaa kwa ajili ya maonesho
tu, hayataruhusiwa kuuza bidhaa hizo kwa kuwa zitakuwa zimeletwa kwa ajili ya
maonesho.
No comments:
Post a Comment