ENTERTAINMENT

ILI KUFIKIA MAFANIKIO KATIKA MAISHA

·         Vijana katika ukanda wa Afrika mashariki watakiwa kutokata tamaa.
·         Ubunifu na kujituma katika kazi yaelezwa ndio nyenzo pekee ya mafanikio: AY.

Na. Deo Kaji Makomba
Katika kuhakikisha vijana wa ukanda wa Afrika mashariki wanafanikiwa katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi, wametakiwa kuwa wabunifu na kutokata tamaa katika shughuli  zao mbalimbali za kila siku za kiujasiliamali, ili waweze kufikia malengo yao.

Ubunifu katika kazi na kutokata tamaa yaelezwa ndio nyenzo pekee ambayo yaweza kuwavusha vijana hao kwenye eneo la ukanda wa  Afrika mashariki katika harakati zao za kila siku za kupambana na maisha.

Changamoto hiyo imetolewa na mwanamuziki wa Tanzania katika muziki wa kizazi kipya, Ambwene Yesaya, almaarufu kama AY,wakati akizungumza katika mahojiano maalum na kisima chetu cha habari kupitia mtandao huu, hivi karibuni.

                                  Mkurugenzi wa Unity Entertainment, Ambwene Yesaya, AY

 AY, katika mahojiano hayo amewataka vijana katika ukanda huu wa Afrika mashariki kutobweteka na maisha waliyonayo na badala yake kuongeza bidii , kupambana katika kazi na kuuchukia umasikini ili kuweza kusonga mbele kimaendeleo zaidi.

Katika falsafa yake ya kujituma na kuwa mbunifu zaidi, AY ameweza kupata mafanikio makubwa kupitia tasinia ya muziki wa kizazi kipya, ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika sekta tofautitofauti, hali iliyompatia manufaa kama yeye binafsi ikiwa ni pamoja  na kutengeneza ajira miongoni mwa vijana wa kitanzania. 

Tangu kuanza muziki kwa AY mnamo miaka ya tisini wakati huo akichomoka na rekodi kadhaa ikiwemo Ni raha tu, Machoni kama watu moyoni hawana utu,zilizomuweka hewani na kudhihirisha kuwa anacho kipaji , amepata mafanikio makubwa akiwekeza katika ardhi, anamiliki kipindi cha TV na kumiliki kampuni ambayo inahusika na masuala mazima ya muziki nchini Tanzania ijulikanayo kwa jina la UNITY ENTERTAINMENT 

Hata hivyo AY, ameongeza kusema kuwa, baadhi ya vijana wamekuwa hawana nidhamu ya kifedha hali inayosababisha baadhi ya taasisi za kifedha kukosa imani na hivyo kushindwa kutoa mikopo ili kuwawezesha katika harakati zao za kupambana na maisha ili kuondokana na umaikini miongoni mwa vijana.

Ndugu msomaji waweza sikiliza mahojiano maalumu kati ya mwanamuziki AY, na kisima cha habari     HAPA….http://www.hulkshare.com/ut7xwzun0kcg

No comments:

Post a Comment