Picha ikionesha mwili wa mwenyekiti wa zamani wa CCM Mkoani Mwanza, marehemu Clement Mabina, aliyepigwa kwa mawe hadi kufa jumapili iliyopita.
TAARIFA KUTOKA IKULU.
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho
Kikwete, amemtumia salam za rambirambi, mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng. Evarist
Ndikilo kufuatia vifo vya watu wawili vilivyotokea decemba 15 2013, katika
kitongoji cha Kanyama Bukelebe kata ya Kisesa wilayani Magu, mkoani Mwanza.
Rais Kikwete ametuma salam
hizo kwa mkuu wa mkoa wa
Mwanza,kufuatia vifo vya Bw. Clement Mabina na Tenery Malimi vilivyotikea baada
ya vurugu zilizosababishwa na mabishano ya ardhi.
Rais amemuomba mkuu wa mkoa huo, kuwatahadharisha wananchi
kutochukua sheria mikononi mwao na pia kuwa waangalifu na matumizi ya silaha za
moto.
“Nimesikitishwa na kufadhahishwa sana na taarifa za vifo vya wananchi
hao wawili (2) vilivyosababishwa na mgogoro wa ardhi ambao ungeweza kupata
suluhu kwa njia za amani. Ni vyema wananchi kuwa na subira na kuwa waangalifu
katika kutatua migogoro yao.” Rais amesema na kuongeza kuwa “ ni vyema subira
na busara zikawa ndio muongozo wa kutatua migogoro yetu katika jamii badala ya
hasira”.
Aidha , Rais Kikwete amemuomba mkuu wa mkoa wa
Mwanza,amfikishie salam za dhati kwa kwa
familia na ndugu wa marehemu Mabina pamoja na Tenery Malimi, ambao walifariki kutokana na
vurugu hizo.
“Amewaomba familia zote mbili ziwe na subira wakati huu mgumu kwa
kuondokewa na wapendwa wao na kuviacha vyombo vya dola kuchukua hatua kwa
kufuata taratibu zilizopo”. Kwa ndugu Mabina , Chama cha mapinduzi
kimepoteza mmoja wa viongozi wake mahiri
na wakutumainiwa. Aidha, kwa marehemu Tenery, taifa limepoteza mmoja wa vijana
wake wanaochipkia ambae angejaliwa kuishi angeweza kutoa mchango muhimu kwa
maendeleo ya jamii na nchi yetu”.
Mabina amewahi kushika nyadhifa mbalimbali, zikiwemo Diwani
na mwenyekiti wa Halmashauri ya Magu mwaka 2000 hadi 2005, mwenyekiti wa chama
cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza, mwaka 2007 hadi 2012.
Rais ameziombea nyoyo za marehemu wote Mungu azilaze mahali
pema peponi Amen.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,
DAR ES ALAAM.