Thursday 27 June 2013

NI MSHIKEMSHIKE HUKO BRAZIL..



NANI KUUNGANA NA BRAZIL KATIKA FAINALI YA KOMBE LA MABARA?

.Ni Italia au Spain?

Na. Deo Kaji Makomba.

Huko nchini Brazil hekaheka za kuwania kombe la mabara leo hii zinatarajiwa kuendelea tena huku kukihuhudiwa mechi nyingine ya nusu fainali ikipigwa.

Mechi  hiyo kati ya timu ya taifa Spain na Itaria, itapigwa kuanzia majira ya saa mbili usiku kwa saa za Afrika mashariki na ndiyo itakayoamua ni timu ipi itakayoungana na Brazil kucheza fainali hizo.

Timu ya taifa ya Uispania ilifanikiwa kuingia hatua ya nusu fanali ya michuano hiyo baada ya kumaliza hatua ya makundi na kushika nafasi ya kwanza katika kundi B na ikijikusanyia pointi tisa kibindoni wakati Italia ikifanikiwa kuingia katika hatua hiyo baada nayo kumaliza hatua ya makundi kwa kujikusanyia pointi sita.

Tayari wenyeji wa mashindano hayo Brazil, wameweza kufanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya hapo jana usiku (Jumatano) kuichakaza timu ya soka ya taifa ya Uruguay, katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza.

Katika mchezo huo Brazil, iliifunga Uruguay mabao 2-1, bao la kwanza likifungwa na mchezaji Fred kunako dakika ya 42 ya mchezo, wakati mlindamlango wa Brazil Cecar awali akiokoa penalty ya Diego Forlan, baada ya David Luiz kumuangusha katika eneo la hatari, nahodha wa timu ya Uruguay, Diego Lugano.
Dakika ya arobaini na nane Uruguay ilinyofoa bao hilo kupitia kwa mchezaji Cavan.

Mpira wa kichwa uliopigwa katika dakika za majeruhi na mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil, Paulinho, ndio uliuuwezesha Brazil kuingia hatua ya fainali , katika mchezo huo uliochezwa kwenye  Estadio Mineirao.
Mechi ya fainali ya michuano hiyo inatarajia kupigwa jumapili hii kwenye uwanja wa Maracana, mjini Reo de Janeiro.

Yafuatayo ni majina ya vikosi vya wachezaji waliocheza mechi hiyo ya nusu fainali ya kwanza kati ya Brazil na Uruguay.

Brazil
  • 12 Julio Cesar
  • 02 Alves
  • 03 Thiago Silva
  • 04 David Luiz Booked
  • 06 Marcelo Booked
  • 11 Oscar (Hernanes - 72' )
  • 17 Dias Booked
  • 18 Paulinho
  • 09 Fred
  • 10 Neymar (Dante - 90' )
  • 19 Hulk (Bernard - 64' )
Uruguay
  • 01 Muslera
  • 02 Lugano
  • 03 Godin
  • 16 Pereira
  • 22 Caceres
  • 07 Rodriguez
  • 17 Arevalo
  • 20 Gonzalez Booked (Gargano - 83' )
  • 09 Suarez
  • 10 Forlan
  • 21 Cavani