wahamiaji haramu kutoka Somalia, wakishushwa kutoka katika lori la mizigo walimokuwa wamejificha.
Wahamiaji haramu
wakamatwa mkoani Morogoro.
·
Ni kutoka
nchini Somalia.
·
Walikuwa
wamejificha katika lori la mizigo.
Na. Mwandishi wetu, Morogoro.
Wahamiaji haramu 16 kutoka nchini Somalia, wamekamatwa
huko mkoani Morogoro, huku wakiwa wamejificha katika lori la mizigo lililokuwa
limebeba chokaa.
Lori hilo lilikuwa likitokea mkoani Tanga, kueleka
mkoani Mbeya.
Kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu, kunatokana na
ushirikiano wa wananchi, ambao umesaidia kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu.
Habari kutoka Mkoani Morogoro zinaeleza kuwa,
kupatikana kwa wahamiaji hao kunafuatia baadhi yao kukosa hewa kutoka na
kujificha kwenye magunia ya chokaa yaliyokuwa yakisafirishwa na lori hilo.
Akizungumza kutoka mkoani Morogoro, kwa upande wake
afisa uhamiaji mkoani humo, Bw. Hamprey Minja, amesema kuwa dereva wa lori hilo
amekamatwa na kufikishwa polisi.