Saturday 12 October 2013

WAHAMIAJI HARAMU KUTOKA SOMALIA



 wahamiaji haramu kutoka Somalia, wakishushwa kutoka katika lori la mizigo walimokuwa wamejificha.
 Wahamiaji haramu wakamatwa mkoani Morogoro.
·     Ni kutoka nchini Somalia.
·     Walikuwa wamejificha katika lori la mizigo.

             
            Na. Mwandishi wetu, Morogoro.


Wahamiaji haramu 16 kutoka nchini Somalia, wamekamatwa huko mkoani Morogoro, huku wakiwa wamejificha katika lori la mizigo lililokuwa limebeba chokaa.

Lori hilo lilikuwa likitokea mkoani Tanga, kueleka mkoani Mbeya.

Kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu, kunatokana na ushirikiano wa wananchi, ambao umesaidia kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu.

Habari kutoka Mkoani Morogoro zinaeleza kuwa, kupatikana kwa wahamiaji hao kunafuatia baadhi yao kukosa hewa kutoka na kujificha kwenye magunia ya chokaa yaliyokuwa yakisafirishwa na lori hilo.

Akizungumza kutoka mkoani Morogoro, kwa upande wake afisa uhamiaji mkoani humo, Bw. Hamprey Minja, amesema kuwa dereva wa lori hilo amekamatwa na kufikishwa polisi.

No comments:

Post a Comment