Saturday 12 October 2013

HEKAHEKA ZA LIGI KUU YA SOKA YA VODACOM TANZANIA BARA.



 Bao pekee la Mkude lazidi kuiweka Simba kileleni.

·     Prions ya Mbeya yatota uwanja wa Taifa
·        Yanga nao wanawili huko Kaitaba, wailaza Kagera Suger  2 - 1

                              

                              Na. Deo Kaji Makomba.

Bao pekee lililotiwa wavuni na mchezaji Jonas Mkude  wa Simba jumamosi hii, limezidi kuwaweka kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya soka ya Vodacom Tanzania bara wekundu hao wa msimbazi Simba.

Simba imezidi kushikilia usukani wa ligi hiyo, baada ya kuwararua maafande wa Tanzania Prions kutoka Mbeya katika moja ya mchezo wa harakati za kuwania ubingwa wa ligi kuu soka ya Vodacom Tanzania bara, uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dare es salaam.

Ilikuwa ni katika kipindi cha pili pale Mkude alipowainua wapenzi na mashabiki wa Simba baada ya kuandika bao pekee na la ushindi, huku goli hilo likionekana kuwa miongoni mwa magoli mazuri kuwahi kutokea katika harakati za mwaka huu za  kuwania ubingwa wa ligi kuu soka ya Vodacom Tanzania bara.

Mkude alifunga bao hilo safi, akiwa katika umbali mrefu kutoka langoni mwa wapinzani wao, akiunganisha mojakwamoja mpira  uliokolewa  kutoka langoni mwa Prisons na hivyo kumuacha mlinda mlango wa Prisons ya Mbeya akiufuata mpira bila mafanikio yoyote.
Kwa matokeo hayo sasa, Simba imefikisha pointi 18 na kuendelea kujikita kileleni mwa ligi hiyo na hivyo kuziacha Azam na Mbeya City kwa tofauti ya pointi Nne.

Nao wapinzani wao wa jadi Dare es salaam young African, wameweza kuibuka na ushindi wa mabao 2 -1 huko kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba walipokuwa wakipambana na wenyeji Kagera Sugera.

 Raundi ya tisa ya ligi hiyo inaanza  Jumapili hii (Oktoba 13 ) kwa mechi kati ya Ruvu Shooting na Rhino Rangers (Mabatini, Mlandizi), Mgambo Shooting na Mbeya City (Mkwakwani, Tanga), Azam na JKT Ruvu (Azam Complex, Dar es Salaam) na Mtibwa Sugar na Oljoro JKT (Manungu, Turiani).

No comments:

Post a Comment