Friday 4 October 2013

BADO NI HATARI HUKO NCHINI MISRI



                         Polisi akiwa amewakamata miongoni mwa wafuasi wa Morsi.

Hali ya hewa huko nchini Misri bado si shwari.

·        Wafuasi wa Morsi kwa mara nyingine wapambana na polisi


·        Usalama waimarishwa Katika medani ya Tahrir
                            
                           
                                Na. deo kaji makomba na mashirika ya habari.

Vikosi vya usalama nchini Misri vimeimarisha ulinzi katika sehemu kadhaa mjini Cairo baada ya vurugu kuzuka kutokana na makabiliano kati ya wafuasi wa Mohammed Morsi na vikosi vya usalama katika mji huo na ule wa Alexandria.

Kwa mujibu wa ripot kutoka katika mashirika mbalimbali ya habari ya kimataifa zinaeleza ya  kuwa milipuko na milio mikubwa ya risasi imesikika katika sehemu za katikati mwa mji mkuu, Cairo.

Kulingana na taarifa hizo, Sehemu ambazo zimezingirwa na polisi ni  zile ambazo wafuasi wa rais aliepindiliwa Mohammed Morsi waliwahi kupiga kambi baada ya Morsi kuondolewa kwa nguvu mamlakani na vikosi vya usalama mwezi Agosti katika operesheni iliyosababisha mamia kadhaa kupoteza maisha.

Pia usalama umeimarishwa karibu na medani ya Tahrir ambako waandamanaji waliokuwa wanapinga Morsi walikusanyika katika maandamano ya kumtaka ajiuzulu kabla ya majeshi kumtoa madarani miezi mitatu iliopita.

 Vyombo vya habari vimeripoti kutokea ghasia zaidi katika mkoa wa Kaskazini wa Sharqiya, Mashariki mwa Gaza, pamoja na Kaskazini mwa mji wa bandarini wa Alexandria.

Mamia ya watu wameuwa tangu jeshi kumuondoa mamlakani Morsi mwezi Julai.

Maelfu ya wanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood pia wamezuiliwa katika miezi miwili iliopita.
Baadhi ya maafisa wakuu wa chama hicho akiwemo bwana Morsi na generali Mohammed Badie, wanazuiliwa kwa madai ya kuchochea ghasia na mauaji.

Wafuasi wa Morsi na vurugu zao huko Misri, wakiendesha harakati zao.

Vuguvugu hilo limelalamika na kusema kuwa maafisa wanazifanya juhudi zao dhidi yao, kuonekana kama vita dhidi ya ugaidi.

No comments:

Post a Comment