Ligi kuu ya soka ya England.
·
Liverpool
Uso kwa uso na Manchester City.
·
Ni katika
mtihani wa kuwania ubingwa wa ligi kuu hiyo.
·
Viwanja
vingine navyo kutimka vumbi Boxing day hii.
Na. Deo Kaji Makomba.
Huko barani ulaya klabu ya soka ya
Liverpool ya England huenda ikasalia kileleni mwa ligi kuu ya soka ya England
katika sikukuu hii ya Krismas, lakini inakabiliwa na mtihani mgumu ili
kujihakikishia kuendelea kukalia kigoda
cha ligi hiyo yenye mashabiki lukuki katika ukanda wa Afrika Mashariki,
watakapokuwa wageni katika Boxing day, mbele ya Manchester City.
Wakiwa katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa
ligi kuu ya kandanda ya England, kwa kuwa na pointi 35 kibindoni, Manchester City wana asilimia kubwa ya kufanya
vizuri katika uwanja wake wa nyumbani wa Etihad, kulingana na rekodi
inavyoonesha hadi hivi sasa katika msimu huu wa ligi kuu hiyo.
Arsenal inayoshikilia nafasi ya pili
katika msimamo wa ligi kuu hiyo itakuwa ugenini leo alhamis boxing day
kupambana na West Ham, wakati Chelsea inayoshikilia nafasi ya Nne watakuwa
wenyeji wa Swansea.
Everton walio katika nafasi ya tano
watapambana na Sunderland nao Mashetani wekundu timu ya Manchester United wako
ugenini kupambana na Hull.
No comments:
Post a Comment